Lugha Nyingine
Mgonjwa wa Ebola apona mjini Goma, mashariki mwa DRC

Wanafamilia wakishangilia ndugu yao kutangazwa kupona baada ya kuwa mgonjwa wa Ebola mjini Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Juni 3, 2026. (Picha na Xinhua)
KINSHASA, Juni 3 — Mgonjwa aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola aliondoka hospitalini siku ya Jumatano huko Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), baada ya kutangazwa kupona na timu za matibabu.
"Tuna furaha sana. Hali yake ilituhangaisha sana. Tangu alipolazwa hospitalini, sisi hatuna hata mmoja aliyeweza kwenda kazini. Sote tulikuwa na wasiwasi sana," alisema Kavira Kazadi, mwanafamilia wa mgonjwa huyo.
Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka ilisema Jumatatu kuwa juhudi za kukabiliana na Ebola katika jimbo la Kivu Kaskazini zinafanyika kwa kufuata mifumo ambayo iliwekwa wakati wa milipuko ya ugonjwa zamani. Jumuiya hiyo ilisema, kituo cha matibabu ya Ebola chenye vitanda 80 kimejengwa mjini Goma, na wagonjwa wa kundi la kwanza wamepokelewa.
Goma, mji mkubwa katika mashariki mwa DRC, umekuwa chini ya udhibiti wa kundi la waasi la M23 tangu mwanzo wa mwaka 2025. Kutokana na kuendelea kwa hali isiyo ya usalama, kuingia katika baadhi ya sehemu za Kivu Kaskazini bado kunakabiliwa na taabu kubwa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema Jumatano kwamba licha ya kukabiliwa na changamoto za usalama na ruhusa za kuingia katika baadhi ya sehemu za mashariki mwa DRC, shirika hilo linaendelea kufanya kazi yake katika eneo la Kivu.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma