Waziri wa mambo ya nje wa Iran asema mapigano yatarejeshwa tena iwapo Israel itashambulia Beirut

(CRI Online) Juni 04, 2026

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Seyed Abbas Araghchi ametoa onyo kuwa kama Israel ikivamia mji wa Beirut nchini Lebanon, jeshi la Iran litajibu kwa kufanya mashambulizi dhidi ya shabaha nchini Israel.

Bw. Araghchi alisema kuwa Iran imeifahamisha pande zote kwa uwazi kwamba ikiwa Israel itaanzisha operesheni za kijeshi dhidi ya Beirut, makubaliano ya kusitisha vita yatachukuliwa kama yamevunjika kabisa, na Iran “haitaivumilia hatua hiyo kamwe”. Pia akibainisha kuwa, Iran imewatahadharisha washirika wake wa kikanda kwamba operesheni zilizopangwa za kijeshi hatimaye zilizuiliwa ili kuepusha mvutano uliopo kuongezeka zaidi.

Akizungumzia hatua iliyofikiwa kwenye mazungumzo kati ya Iran na Marekani, Bw. Araghchi alisema kuwa ingawa mawasiliano na Marekani hayajakoma, hakuna maendeleo makubwa yaliyofikiwa. Alisisitiza kuwa masharti ya kurejea katika meza ya mazungumzo lazima yalinde maslahi ya Iran, kukomesha mapigano nchini Lebanon na kusitisha kuongezeka kwa mivutano ya kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha