Lugha Nyingine
Mkuu wa WHO asema mwitikio wa Ebola nchini DRC wapata maendeleo
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema katika mkutano na wanahabari huko Geneva Jumatano kwamba kutokana na juhudi na uratibu wa pamoja, mwitikio wa mlipuko unaoendelea wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaongezeka.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye amerejea kutoka ziarani DRC, alisema alitiwa moyo sana na kiwango cha kujitolea alichokiona nchini humo ingawa changamoto bado zipo.
Tedros alisema kuwa nchini DRC, visa 344 wamethibitishwa, ikiwa ni pamoja na vifo 60, kwenye maeneo 24 ya afya katika majimbo matatu, huku idadi ya watu wanaoshukiwa kuambukizwa ikipungua hadi 116 kutoka zaidi ya 1,000 wiki iliyopita.
Tedros alisema tathmini ya hatari ya WHO bado haijabadilika: iko juu sana katika ngazi ya kitaifa, juu katika ngazi ya kikanda, na chini katika ngazi ya kimataifa. Alisema mlipuko huo ulianza kwa kasi, na bado wako nyuma, lakini chini ya uongozi wa Serikali ya DRC, wanapata maendeleo.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma