Lugha Nyingine
China kushiriki katika uteuzi wa katibu mkuu wa awamu ijayo wa UN kwa njia ya kuwajibika na ya kiujenzi

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), jana Tarehe 4, Juni hapa Beijing akikutana na Michelle Bachelet, mgombea wa nafasi ya katibu mkuu anayefuata wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye pia ni Rais wa zamani wa Chile. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana hapa Beijing amekutana na Michelle Bachelet, mgombea wa nafasi ya katibu mkuu anayefuata wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye pia ni Rais wa zamani wa Chile.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema kwamba China itashiriki katika uteuzi wa katibu mkuu wa awamu ijayo wa Umoja wa Mataifa kwa njia ya kuwajibika na ya kiujenzi, na itafanya juhudi za kuhimiza Umoja wa Mataifa kurudia katika hali yake yenye heshima na mamlaka na nguvu hai, ili kuendana na hali mpya ya kimataifa na kukabiliana na changamoto mpya.
Bachelet ameuelezea Umoja wa Mataifa kuwa ni jukwaa lisilo na mbadala kwa jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana kwa pamoja na changamoto duniani, akisema Umoja wa Mataifa unapaswa kuhifadhi heshima na mamlaka ya Katiba yake, kushikilia mwelekeo wa kivitendo na kuchukua hatua za maoni ya kauli moja zilizoratibiwa ili kusukuma mbele nguzo kubwa tatu za amani, maendeleo na haki za binadamu.
Akisisitiza ahadi yake ya uthabiti juu ya kanuni ya kuwepo kwa China moja, Bachelet ameelezea pongezi zake kwa juhudi za muda mrefu za China katika kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi na mambo ya Umoja wa Mataifa, na pia amesema anapenda kushirikiana pamoja na China na jumuiya ya kimataifa katika kuinua hadhi na umuhimu wa Umoja wa Mataifa.
Wang Yi amesema kuwa siku zote China ni muungaji mkono mkubwa na mjenzi mwenye juhudi za mambo ya Umoja wa Mataifa, China inapenda kushirikiana na pande zote katika kulinda, kustawisha na kuimarisha Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), jana Tarehe 4, Juni hapa Beijing akikutana na Michelle Bachelet, mgombea wa nafasi ya katibu mkuu anayefuata wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye pia ni Rais wa zamani wa Chile. (Xinhua/Yue Yuewei)

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma