Lugha Nyingine
ChinaVumbuzi | Wanasayansi wa China watengeneza mahindi yenye protini nyingi kwa malisho ya mifugo

Mtafiti akiandaa sampuli za mahindi ndani ya maabara ya Kituo cha Ubora wa Sayansi za Molekuli za Mimea (CEMPS) cha Akademia ya Sayansi ya China (CAS), Shanghai, mashariki mwa China, Juni 2, 2026. (Xinhua/Jin Liwang)
SHANGHAI - Wanasayansi wa China wamegundua jeni mbili muhimu zinazochangia kiwango kikubwa cha protini katika mahindi na wamefanikiwa kutengeneza aina mpya za mahindi zenye protini nyingi, wakitoa suluhisho lenye matumaini kwa uhaba wa protini ya malisho ya mifugo nchini China.
Mahindi ni zao la nafaka linalozalishwa kwa wingi zaidi nchini China, hata hivyo, kiwango chake cha protini kwa ujumla ni cha chini, kikiwa asilimia karibu 8 pekee, hali inayosababisha utegemezi mkubwa wa unga wa soya unaoagizwakutoka nje kama chanzo cha protini kwa mifugo, kwa mujibu wa Wu Yongrui, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Ubora wa Sayansi za Molekuli za Mimea (CEMPS) cha Akademia ya Sayansi ya China (CAS).
"Kwa hivyo, kutengeneza mahindi yenye protini nyingi ili kuchukua nafasi ya unga wa soya ulioagizwa kutoka nje katika malisho ya mifugo ni mbinu yenye matumaini katika kukabiliana na upungufu wa protini ya malisho nchini. Hata hivyo, kwa muda mrefu, juhudi za uboreshaji wa mbegu hazikuwa na upatikanaji wa jeni bora zenye protini nyingi," Wu amebainisha.
Mwaka 2022, timu ya utafiti iliyoongozwa na Wu ilitambua jeni ya kwanza yenye protini nyingi, THP9-T, kutoka kwenye mahindi pori. Kupitia juhudi zisizokoma, timu hiyo imebaini kwa mafanikio jeni ya pili yenye protini nyingi, THP3-T. Wu amebainisha kuwa, majaribio ya miaka mingi ya shambani yameonyesha kuwa jeni hiyo inaweza kuongeza kiwango cha protini ya punje kutoka asilimia 10 hadi zaidi ya asilimia 13 ndani ya aina za kujichavusha za mbegu bila kupunguza mavuno.

Watafiti wakifanya shughuli za uchavushaji kwenye mahindi katika shamba la Kituo cha Ubora wa Sayansi za Molekuli za Mimea (CEMPS) cha Akademia ya Sayansi ya China (CAS), Shanghai, mashariki mwa China, Juni 2, 2026. (Xinhua/Jin Liwang)

Mtafiti akitoa DNA kutoka kwenye sampuli za mahindi katika maabara ya Kituo cha Ubora wa Sayansi za Molekuli za Mimea (CEMPS) cha Akademia ya Sayansi ya China (CAS), Shanghai, mashariki mwa China, Juni 2, 2026. (Xinhua/Jin Liwang)

Picha iliyopigwa Juni 2, 2026 ikionyesha mkutano na waandishi wa habari wa mafanikio ya utafiti katika Kituo cha Ubora wa Sayansi za Molekuli za Mimea (CEMPS) cha Akademia ya Sayansi ya China (CAS), Shanghai, mashariki mwa China, Juni 2, 2026. (Xinhua/Jin Liwang)

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma