Xi asema uhusiano kati ya China na DPRK unakabiliwa na fursa mpya na jukumu jipya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2026

BEIJING – Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema, kwa sasa, uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) uko katika hatua mpya ya mwanzo kihistoria, ukikabiliwa na fursa mpya za maendeleo na kubeba jukumu jipya la zama.

Rais Xi ameyasema hayo leo Jumatatu kwenye makala yake iliyochapishwa kwenye gazeti la Rodong Sinmun, ambalo ni gazeti la kiserikali la DPRK, kabla ya ziara yake ya kiserikali nchini DPRK iliyopangwa kufanyika Jumatatu na Jumanne, hii ni ziara yake ya kwanza nchini humo katika miaka saba iliyopita.

Xi akisema kuwa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano kati ya China na DPRK siku zote kumekuwa sera ya utekelezaji wa kithabiti ya chama cha CPC na serikali ya China, China inapenda kushirikiana na DPRK katika kuhimiza uhusiano wa pande mbili kwa mtazamo wa kimkakati, kuufanya uhusiano kati ya China na DPRK uendane na wakati, na kufikia maendeleo makubwa zaidi ya uhusiano huo.

"Pande hizo mbili zinapaswa kuzidisha mawasiliano ya kimkakati na kuongeza maelewano, na kuuelekeza kithabiti uhusiano kati ya China na DPRK kwa mwelekeo sahihi," Rais Xi amesema, akitoa wito wa kushikilia desturi nzuri ya mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya vyama viwili na nchi hizo mbili, na kudumisha mawasiliano ya karibu kama familia moja.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuchukua maadhimisho ya miaka 65 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Urafiki, Ushirikiano na Kusaidiana kati ya China na DPRK kuwa fursa ya kuimarisha mawasiliano kwenye ngazi zote na katika vyombo vya chama, serikali na jeshi, kutekeleza maoni muhimu ya kauli moja yaliyofikiwa na pande hizo mbili, na kuongeza msukumo mpya kwa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

Rais Xi amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano na kufundishana ili kuhimiza kwa pamoja mambo ya ujamaa ya nchi hizo mbili yaendelezwe kwa hatua madhubuti.

Pia ametoa wito wa kufanya uratibu wa karibu wa pande nyingi na kulinda kithabiti haki na usawa wa kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha