Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini atangaza mpango wa kukabiliana na uhamiaji haramu
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza mfululizo wa hatua zinazolenga kukabiliana na uhamiaji haramu kufuatia wasiwasi unaoongezeka wa umma juu ya suala hilo.
Akihutubia taifa jana Jumapili mjini Pretoria, Rais Ramaphosa amesema baraza la mawaziri limepitisha mbinu za kina za usimamizi wa uhamiaji, zinazolenga kuimarisha utekelezaji wa shughuli za uhamiaji, kuhakikisha usalama wa mipaka, kupambana na ufisadi, na kuboresha mfumo na sera za uhamiaji.
Amesema chini ya mbinu hizo mpya, serikali itaongeza juhudi za kuwatambua na kuwarejesha nyumbani wahamiaji wasio na utambulisho rasmi, kuanzisha mahakama maalumu za uhamiaji ili kuharakisha mchakato wa kuwarejesha nyumbani wahamiaji hao, kuimarisha usalama wa mipaka, na kuweka faini kali zaidi kwa waajiri ambao wanaajiri wageni wasio na utambulisho rasmi kwa makusudi.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma