Lugha Nyingine
Iran yarusha makombora nchini Israel kwa mara ya kwanza tangu usimamishaji mapigano mwezi Aprili

Picha hii iliyopigwa Februari 28, 2026 ikionyesha njia za makombora ya kuzuia mashambulizi yaliyorushwa kutoka mifumo ya ulinzi wa anga ya Israeli, Tel Aviv, Israel. (Xinhua/Chen Junqing)
JERUSALEM/TEHRAN - Iran jana Jumapili jioni ilirusha mawimbi kadhaa ya makombora dhidi ya Israel na kuionya Israel isilipize kisasi, katika mashambulizi ya kwanza ya namna hiyo tangu makubaliano ya kusimamisha mapigano kufikiwa mwezi Aprili.
Makombora hayo yalisababisha ving'ora kote kaskazini mwa Israel. Hadi sasa hakuna taarifa za majeruhi au uharibifu. Mkuu wa Majeshi wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Eyal Zamir amesema jeshi "litamshambulia adui kwa nguvumara tu amri itakapotolewa."
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran kimethibitisha katika taarifa kwamba kililenga Kituo cha Anga cha Ramat David cha Israel kwa makombora ya balestiki kukabiliana na "uhalifu wake mkubwa" nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars ambalo linamilikiwa kwa kiasi fulani na serikali ya Iran, Kamanda Mkuu wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya ya Iran Ali Abdollahi amesema Jumapili usiku kwamba kama Israeli itapanua mashambulizi yake kusini mwa Lebanon na eneo la Dahieh kusini mwa Beirut, au kujibu hatua hizo za Iran, itakabiliwa na "mapigo makali zaidi na ya kuwafanya wajute."
Katika taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo Jumatatu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kwamba vikosi vya jeshi la Iran vimeshambulia shabaha kadhaa ndani ya Israeli usiku uliotangulia ndani ya mfumo wa haki halali ya nchi hiyo ya kujilinda, kufuatia "vitendo vya uchokozi" vya mara kwa mara vya Israeli dhidi ya Lebanon na Iran na ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya kusimamisha mapigano ya Aprili.
Msemaji wa IDF Effie Defrin amesema kwamba Iran imefanya "kosa kubwa" kwa kurusha makombora dhidi ya Israeli, akiongeza kwamba jeshi limejiandaa kwa uwezekano wa makombora zaidi.
Mashambulizi hayo ya Iran yamekuja baada ya Israeli kuanzisha mashambulizi ya anga katika vitongoji vya kusini mwa Beirut mapema siku hiyo, ambapo Kituo cha Uendeshaji wa Dharura ya Afya ya Umma cha Lebanon kimesema yameua watu wasiopungua wawili na kujeruhi wengine 20.

Picha iliyopigwa Juni 2, 2026 ikionyesha waokoaji wakifanya kazi kwenye magofu ya majengo ya makazi baada ya shambulio la anga la Israeli katika mji wa Tyre, kusini mwa Lebanon. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)
Iraqi militia Kata'ib Hezbollah, an ally of Iran, threatened on Sunday night to attack U.S. military bases and interests if the United States strikes Iran, while Yemen's Houthi group voiced support for the Iranian attacks against Israel.
Wanamgambo wa Iraqi Kata'ib Hezbollah, ambao ni washirika wa Iran, wametishia jana Jumapili usiku kushambulia kambi za kijeshi na maslahi ya Marekani kama Marekani itaishambulia Iran, wakati huhuo kundi la Wahouthi la Yemen limeelezea uungaji mkono kwa mashambulizi hayo ya Iran dhidi ya Israeli.
Katikati ya hali ya mvutano huo mpya wa kikanda, Iraq imetangaza jana Jumapili usiku kufungwa kwa muda kwa anga yake kwa ndege zote kwa saa 72 ikiwa ni hatua ya tahadhari. Syria imesema imefunga njia zake za anga za kusini kwa saa 12 na kusimamisha shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus.
Akizungumzia shambulio hilo la Iran, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumapili kwamba alikuwa akipanga kumpigia simu Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kumhimiza asijibu mashambulizi hayo kwa sababu hakutaka mazungumzo ya kusimamisha mapigano kati ya Marekani na Iran yavunjike, kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Channel 12 cha Israeli.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma