Lugha Nyingine
Rwanda yajitayarisha kukabiliana na mlipuko wa Ebola unaoweza kutokea
Waziri Mkuu wa Rwanda Justin Nsengiyumva amesema, nchi hiyo imeweka hatua za kuzuia, ufuatiliaji na matibabu ili kukabiliana na mlipuko wowote wa Ebola unaoweza kutokea nchini humo, huku ikilinda afya ya umma na shughuli za kiuchumi.
Bw. Nsengiyumva amesema hayo Jumamosi iliyopita wakati akitoa taarifa kwa wanahabari huko Kigali, mji mkuu wa Rwanda.
Amesema, wana uhakika kwamba wana vifaa vya kulinda maisha ya raia bila ya kuvuruga shughuli za kijamii na kiuchumi, huku akitoa wito kwa wakazi kuwa na tahadhari, kuhakikisha usafi na kumripoti mtu yeyote wanayemshuku.
Akizungumza katika mkutano huohuo na wanahabari, waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Sabin Nsanzimana ameeleza kuwa nchi hiyo imejenga uwezo katika nyanja tano, zikiwemo za mawasiliano, ufuatiliaji, uwezo wa utambuzi, uwezo wa kufuatilia watu waliokutana na watu wanaoshukiwa kuambukizwa na usimamizi wa wagonjwa kwa kupitia vituo vya matibabu vilivyozinduliwa.

Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini

Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini yaadhimisha miaka 100

Nishati ya kijani yahimiza maendeleo yenye sifa bora katika Mkoa wa Xizang, China

Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma