WHO yasema mlipuko wa Ebola unaenea kwa kasi nchini DRC hata hadi Uganda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2026

Wafanyakazi waandaa chakula kwa watu walio chini ya karantini mjini Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), tarehe 4 Juni 2026. (Xinhua)

Wafanyakazi waandaa chakula kwa watu walio chini ya karantini mjini Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), tarehe 4 Juni 2026. (Xinhua)

GENEVA - Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaenea kwa kasi, ambapo idadi ya wagonjwa imeongezeka, na maambukizi yake yamefikia sehemu mbalimbali tofauti ya kijiografia hata yamevuka mpaka hadi Uganda.

Katika taarifa yake mpya zaidi ya jana Jumatatu, WHO imesema kwa sasa shirika hilo linatathmini hatari ya maambukizi nchini DRC ni ya juu sana, Uganda na maeneo yaliyoathiriwa ya nchi jirani yanayopakana kwa ardhi yanakabiliwa na hatari ya juu, na nchi nyingine za bara la Afrika na maeneno mengine duniani yanakabiliwa na hatari ya chini.

Hadi kufikia Jumapili, DRC ilikuwa imeripoti wagonjwa 515 waliothibitishwa, ikiwa ni pamoja na vifo 91 vya watu. Uganda ilikuwa imeripoti wagonjwa 19 waliothibitishwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya watu wawili na mwingine mmoja anayedhaniwa kufariki kutokana na ebola.

Wagonjwa wote nchini Uganda wanahusika na mlipuko huo nchini DRC kwa maambukizi yake ya kimaeneo, huku kukiwa na ushahidi wa maambukizi yaliyoingizwa kutoka nje na maambukizi ya pili miongoni mwa watu waliokutana nao na wafanyakazi wa afya.

Mamlaka za nchi mbalimbali, zikifanya kazi pamoja na WHO na washirika, zinatekeleza hatua mbalimbali za kukabiliana na hali ya maambukizi ya virusi. Juni 5, Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa na WHO vilianzisha mpango wa pamoja wa bara zima wa kujiandaa na kukabiliana na Ebola, vikitafuta dola milioni 518 za Marekani kwa kuunga mkono nchi za Afrika katika maandalizi, upimaji na kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Mlipuko huo unahusika na ugonjwa wa virusi vya Bundibugyo (BVD), aina kali ya ugonjwa wa Ebola ambao unasababisha mara kwa mara vifo vya watu. Virusi hivyo vinaaminika kuwa vinatoka kwenye popo wa matunda na vinaweza kuenea kupitia kukutana kwa karibu na damu au ute wa wanyama walioambukizwa au majimaji ya mwili wa watu walioambukizwa.

Kipindi cha kuzaliana na kukomaa kwa BVD ni kati ya siku mbili hadi 21, na watu walioambukizwa hawawezi kuambukiza hadi dalili zionekane. 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha