Kenya yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu kwa wito wa mshikamano (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2026
Kenya yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu kwa wito wa mshikamano
Zainab Hawa Bangura, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi (UNON), akizungumza katika sherehe ya mada ya Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu jijini Nairobi, Kenya, Juni 10, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)

NAIROBI - Sherehe ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu imefanyika Nairobi, mji mkuu wa Kenya, Jumatano, ikiwakutanisha maafisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia na wasomi.

Katika hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres iliyotolewa kwa niaba yake na Zainab Hawa Bangura, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi (UNON), Guterres amesema kwamba ingawa tofauti mara nyingi hufanyiwa udanganyifu ili kudhoofisha mshikamano duniani, mazungumzo yanabaki kuwa njia pekee inayofaa ya maelewano kati ya mataifa, tamaduni na imani tofauti.

"Katika maadhimisho haya ya pili ya Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu, tunatambua nguvu ya mawasiliano ya wazi katika kutatua hata changamoto ngumu zaidi duniani. Tunaposikiliza, kuzungumza na kuungana, ushirikiano huwa mbadala wa mapambano na uaminifu huwa mbadala wa mvutano," amesema.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja azimio lililofadhiliwa na China Juni 2024 likiitangaza Juni 10 kuwa Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu.

Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan amesema kwamba mazungumzo kati ya ustaarabu huunda msingi wa mabadilishano ya kitamaduni na ya kati ya watu na watu, akibainisha kuwa Pendekezo la Ustaarabu Duniani la China linahimiza kuelewana na mapatano miongoni mwa ustaarabu mbalimbali.

Ameongeza kuwa kufunzana miongoni mwa ustaarabu kutazalisha ushirikiano na kusaidia kuharakisha maendeleo katika nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Guo, mapendekezo manne ya kimataifa ya China kuhusu maendeleo, usalama, ustaarabu na utawala yameingiza utulivu na uhakika katika dunia yenye hali tete, an kutoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

Shughuli hiyo ilimalizika kwa kuonyeshwa kwa filamu ya Kichina "Tale of the Night" ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Filamu ya Hunan nchini Kenya, ambayo inalenga kuhimiza mazungumzo ya kati ya tamaduni, urafiki na kuelewana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha