Lugha Nyingine
China yasema kurudisha haraka usalama na uhuru wa usafiri kwenye Mlango Bahari wa Hormuz kunaendana na maslahi ya pande zote
(CRI Online) Juni 17, 2026
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesema, Mlango Bahari wa Hormuz unatumika kwa usafiri wa kimataifa, na kwamba kurudisha haraka usalama na uhuru wa usafiri kwenye mlango huo kunaendana na maslahi ya pande zote.
Lin Jian ameyasema hayo Jumanne wakati akizungumzia makubaliano ya awali ya hatua ya mwanzo kuhusu kufungua tena Mlango Bahari wa Hormuz yaliyofikiwa kati ya Iran na Marekani.
Lin Jian amesisitiza kuwa, China iko tayari kudumisha mawasiliano na nchi husika na jumuiya ya kimataifa, na pia itaendelea kulinda usalama wa meli na wafanyakazi wa meli wa China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



