Afrika Kusini yaadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana kwa kutoa heshima kwa wanafunzi wa Soweto wa mwaka 1976

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2026

Picha hii iliyopigwa Juni 16, 2026 ikionyesha mwonekano wa hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini. (Xinhua/Chen Wei)

Picha hii iliyopigwa Juni 16, 2026 ikionyesha mwonekano wa hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini. (Xinhua/Chen Wei)

JOHANNESBURG - Afrika Kusini imeadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana jana Jumanne, ikikumbuka miaka 50 ya Uasi wa Soweto wa mwaka 1976, ambao ni wakati muhimu katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Hafa hiyo rasmi imefanyika kwenye Uwanja wa FNB Premium Parking Precinct mjini Johannesburg, ambapo Rais Cyril Ramaphosa alitoa hotuba kuu.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kushoto) akihutubia hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 16, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kushoto) akihutubia hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 16, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Ramaphosa ametoa heshima kwa vijana hao wa mwaka 1976, akisifu ujasiri na kujitoa mhanga kwao. Amesema vitendo vyao vilisaidia kubadilisha mwelekeo wa kupinga ubaguzi wa rangi na kuvutia ufuatiliaji wa watu wa kote duniani juu ya vitendo vya mabavu vya utawala baada ya kuona picha za watoto wa shule waliojeruhiwa na kuuawa zilizotangazwa.

"Walikumbana na risasi kwa mikono mitupu. Walipinga hali isiyo ya usawa na haki wakiwa kwa ujasiri wa ajabu. Na kwa kupitia kujitolea mhanga kwao, walibadilisha mchakato wa historia ya nchi yetu," amesema.

Siku ya Kitaifa ya Vijana ya 2026 inaadhimisha miaka 50 tangu maelfu ya wanafunzi wa Soweto walipoandamana mitaani kupinga serikali ya ubaguzi wa rangi kuwalazimisha watoto weusi kutumia lugha ya Kiafrikana katika masomo darasani.

“Serikali hiyo ya ubaguzi wa rangi ilikuwa imeharibu elimu ya watoto Weusi kwa kupitia Sheria ya Elimu ya Wabantu mapema mwaka 1953 na mtaala wake duni,” Ramaphosa amesema, akiongeza kuwa kuanzishwa kwa lugha ya Kiafrikana kuwa lugha ya kufundishia kukawa kichocheo cha upingaji wa watu katika maeneo mbalimbali.

Maelfu ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walijiunga na maandamano hayo, ambayo yalikabiliwa na mabomu ya machozi na risasi za bunduki kutoka kwa polisi.

Katika hotuba yake kuu, Ramaphosa amesema vijana hao wa mwaka 1976 walifanya mapambano dhidi ya ukandamizaji wa ubaguzi wa rangi na mfumo wa elimu usio wa usawa na haki, na vijana wa hivi leo wanakabiliwa na changamoto tofauti, zikiwemo za ukosefu wa ajira na hali isiyo ya usawa. Amesema ukosefu wa ajira kwa vijana nchini humo ni asilimia 46, huku vijana zaidi ya milioni 4.7 wakiwa hawana ajira.

“Chanzo cha Changamoto zinazowakabili vijana hivi leo kinatokana na hali isiyo na usawa iliyo ya kina zaidi na ukuaji wa uchumi uliodumaa,” amesema, akiongeza kuwa kuzishughulikia changamoto hizo kunahitaji hatua za “pande zote na za dharura”.

Ramaphosa amesema serikali inapanua ajira za umma, huduma kwa vijana na uzoefu wa mahali pa kazi ili kupambana na changamoto hizo zinazowakabili vijana.

"Ukosefu wa ajira lazima uchukuliwe kuwa ni tatizo la jamii. Wadau wote katika nchi yetu lazima wafanye juhudi za pamoja ili kutoa mpango wa utatuzi endelevu ili kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana," ameongeza. 

Wasanii wakifanya maonesho kwenye hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 16, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Wasanii wakifanya maonesho kwenye hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 16, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Wanafunzi wakipiga picha pamoja kwenye hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 16, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Wanafunzi wakipiga picha pamoja kwenye hafla rasmi ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Vijana, huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 16, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha