Lugha Nyingine
Mjumbe wa China ahudhuria mkutano maalum kuhusu kukabiliana na Ebola barani Afrika
Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China Liu Guozhong, amehudhuria na kuhutubia Mkutano Maalum kuhusu Kukabiliana na Ebola Barani Afrika uliofanyika kwa njia ya video jana Jumanne.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Liu amesema, China imetoa usaidizi wa dharura wa kibinadamu kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Umoja wa Afrika, imepeleka timu ya wataalamu wa matibabu nchini DRC ambao wanashirikiana na wataalamu wa Afrika kupambana na janga hilo.
Mkutano huo uliitishwa na Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, na kuhudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali kutoka zaidi ya nchi kumi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Guinea ya Ikweta, na Zimbabwe, pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa na ya kikanda kama vile Shirika la Afya Duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



