Timu ya madaktari wa China yatoa huduma ya matibabu bila malipo Tanzania Zanzibar

(CRI Online) Juni 18, 2026

Kundi la 35 la timu ya madaktari wa China Tanzania Zanzibar jana Jumatano imetoa huduma ya bila malipo ya matibabu kwenye Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Kidundo katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, kwa kutoka huduma za afya na mahitaji muhimu kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Mpango huo, ambao ni sehemu ya mradi wa China wa "Timu 100 za madaktari katika Vijiji 1,000," ulijikita katika kuboresha afya na ustawi wa watoto wanaoishi chini ya uangalizi wa kitaasisi.

Wataalamu wa matibabu ya magonjwa ya ndani ya mwili, meno, ngozi, macho na magonjwa ya masikio na koo walifanya vipimo vya kina vya afya vilivyohusisha magonjwa kama utapiamlo, maambukizi kwenye mfumo wa hewa, matatizo ya kuona na masuala ya afya ya kinywa.

Timu hiyo pia imetoa vifaa vya mahitaji ya kila siku, vifaa vya shule na michezo, huku ikishirikiana na watoto kupitia michezo na shughuli mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha