Maonyesho ya kazi ya China-Tanzania yawaunganisha vijana na fursa za ajira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2026

Watafuta kazi wakijaza fomu za maombi ya kazi kwenye banda katika Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 16, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Watafuta kazi wakijaza fomu za maombi ya kazi kwenye banda katika Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 16, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - Asubuhi yenye manyunyu Jumanne, mamia ya vijana wa Tanzania walimiminika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania. Walikusanyika kwa ajili ya Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania, shughuli ya siku moja iliyokutanisha watafuta kazi na waajiri kutoka sekta mbalimbali.

Huku kampuni zaidi ya 60 za China zikiwa zimeshiriki katika sekta kuanzia ujenzi na uzalishaji bidhaa hadi teknolojia ya kupashana habari na mambo ya fedha, maonyesho hayo yametoa njia ya kupata ajira kwa watafuta kazi wenye shauku ya kujenga mustakabali wao.

Miongoni mwao ni Bwakea Bandeko mwenye umri wa miaka 39, ambaye alihitimu shahada ya kwanza katika utalii na urithi wa kitamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka 2013. Kama ilivyo kwa wengine wengi, Bandeko alitembea kutoka banda moja hadi jingine, akiwa na CV mkononi, akiwa mwenye matumaini lakini pia mwenye mtazamo wa uhalisia.

"Nimetembelea kampuni zaidi ya 20 hadi sasa," amesema. "China ina kampuni kubwa sana zinazowekeza nchini Tanzania. Ninaamini kuna nafasi kubwa ya kupata kazi."

Shughuli hiyo "imekuja kwa wakati sahihi, kwani inawaunganisha vijana na fursa halisi," ameongeza.

Katika viwanja vya maonyesho hayo, mistari ilipangwa mbele ya mabanda ya kampuni, ambapo waajiri walishiriki na watafuta kazi katika mahojiano mafupi na kukusanya wasifu. Mazungumzo yalifanyika kwa Kiingereza, Kiswahili na, kwa hali inayoongezeka, lugha ya Kichina, ambayo ni ishara ya uhusiano unaopitia hali mbalimbali kati ya mataifa hayo mawili.

Maonyesho hayo, yaliyofanyika chini ya kaulimbiu ya "Kuunganisha Vipaji, Kutoa Fursa, Kujenga Mustakabali Wetu Pamoja," yaliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Tanzania, Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina nchini Tanzania, na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akifungua shughuli hiyo, Waziri wa Nchi wa Tanzania katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na Kazi, Ajira na Uhusiano Deus Clement Sangu amesema maonyesho hayo ni ishara ya ushirikiano na ustawi wa pamoja.

"Shughuli hii inawakilisha fursa, ushirikiano na nia ya pamoja kwa mataifa yetu mawili kuwekeza katika watu," amesema.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema maonyesho hayo ya kazi "yanaonyesha dhamira yetu ya pamoja kwa ushirikiano na maendeleo ya pamoja."

Amesema kwamba kampuni za China nchini Tanzania zinatumika si tu kama vichocheo vya ukuaji wa uchumi bali pia kama madaraja yanayounganisha watu na tamaduni.

Mwajiri akitumia kompyuta ya mkononi kuonyesha maelezo ya kazi na taarifa za kampuni kwa waombaji kazi kwenye Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 16, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Vijana wa Tanzania wakiwa wamekusanyika kwenye banda kuuliza kuhusu fursa za ajira kwenye Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 16, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Waajiri wakizungumza na watafuta kazi kwenye Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 16, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Waajiri wakizungumza na watafuta kazi kwenye Maonyesho ya tano ya Kazi ya China na Tanzania jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 16, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha