Lugha Nyingine
Mjumbe wa China asema Pendekezo la Usimamizi Duniani linatoa suluhisho kwa usimamizi duniani

Jia Guide, Mjumbe wa kudumu ambaye pia ni Balozi wa China kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi, akihudhuria mjadala usio rasmi wa ngazi ya juu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa Baraza la Haki za Binadamu, mjini Geneva, Uswisi, Juni 19, 2026. (Xinhua/Wang Qibing)
GENEVA – Jia Guide, Mjumbe wa kudumu ambaye pia ni Balozi wa China kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi amesema pendekezo la Usimamizi Duniani linalopendekezwa na China linatoa suluhisho la China kwa nakisi ya usimamizi duniani na linatoa mwanga mpya juu ya namna ya kuimarisha na kuboresha kazi ya Baraza la Haki za Binadamu la UN.
Balozi Jia ameyasema hayo kwenye mjadala usio rasmi wa ngazi ya juu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa Baraza la Haki za Binadamu, mjini Geneva, Uswisi siku ya Ijumaa kwenye mkutano wa 62 wa baraza hilo.
Amesema kuwa maadhimisho hayo ya miaka 20 tangu kuanzishwa Baraza la Haki za Binadamu ni wakati muhimu wa kudhamiria tena kwa matarajio ya awali ya baraza hilo, kutafakari yaliyopo na kutazama mbele kwa siku za baadaye.
Amesema kuimarisha na kuboresha kazi ya baraza hilo kunahitaji kushikilia kanuni za usawa wa mamlaka ya nchi na utawala wa sheria wa kimataifa.
"Baraza linapaswa kuongozwa na kanuni za ujumuishaji wote, kutokuwa na upande, kutoegemea upande, kutochagua, na mazungumzo na ushirikiano wa kujenga, na kupinga kuingiza mambo ya kisiasa. Pia linahitaji kushikilia mbinu inayotilia maanani watu, kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi," amesema Balozi Jia.
Amesema Baraza hilo linapaswa kuhimiza maendeleo yenye uwiano kati ya haki za kiraia na kisiasa pamoja na haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni, na kuweka haki za maendeleo juu zaidi kwenye ajenda ya haki za binadamu ya pande nyingi.
"Zaidi ya hayo, inahitaji mbinu yenye mwelekeo wa vitendo, kuhimiza manufaa kwa wote na ya usawa. Baraza linapaswa, kwa kuzingatia idhini ya nchi husika, kuwekeza zaidi katika ujengaji uwezo na usaidizi wa kiufundi."
Akibainisha kuwa ustaarabu upo katika utofauti mkubwa, Balozi Jia amesema njia ya maendeleo ya haki za binadamu ya kila nchi iliyochaguliwa nao wenyewe inastahili heshima kamili. "Lazima tuelewe kwa usahihi uhusiano kati ya haki za binadamu za kidunia kwa wote na utofauti wa ustaarabu," amesema.
"China inathamini uhimizaji na ulinzi wa haki za binadamu, na inafuata bila kuyumba njia ya maendeleo ya haki za binadamu ya China,” Jia amesema, akiongeza kuwa China iko tayari kushirikiana na mataifa yote ili kusukuma mbele maendeleo mazuri ya shughuli za haki za binadamu duniani na kusaidia kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



