Lugha Nyingine
Rais Xi na Rais wa Ushelisheli watumiana salamu za kupongeza maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa nchi mbili
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Ushelisheli Patrick Herminie wametumiana salamu za kupongeza maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Kwenye salama zake zilizotolewa jana Jumanne, Xi amesema kwamba katika miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, China na Ushelisheli siku zote zinaamiana, na kuungana mkono kithabiti bila kujali hali ya kimataifa inavyobadilika namna gani, na urafiki kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuwa imara tangu mwanzo mpaka sasa.
Xi ameeleza imani yake thabiti kwamba ilimradi pande zote mbili zitashikilia nia ya awali ya kuanzishwa kwa uhusiano huo wa kidiplomasia na kusonga mbele bega kwa bega, njia ya uhusiano kati ya China na Ushelisheli itakua pana zaidi na matarajio kwa ushirikiano wa pande mbili yatakuwa angavu zaidi.
Akisema kwamba anaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ushelisheli, na China inapenda kufanya ushirikiano na Herminie ili kuchukua maadhimisho hayo ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kuwa mwanzo wa kuenzi urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili.
Xi pia ameahidi kufanya juhudi za pamoja na Herminie katika kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana ndani ya mifumokazi ya ushirikiano wa sifa bora katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuhimiza maendeleo kwa pamoja, ili kuinua ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ushelisheli kwenye kiwango cha juu, na kuleta manufaa mengi zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Herminie amesema katika salamu zake za pongezi kwamba, katika miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya Ushelisheli na China umeendelea kuimarika kwa hatua madhubuti kweye msingi wa kuheshimiana, kuaminiana na kutafuta maendeleo kwa pamoja.
"China siku zote ni mshirika muhimu kwa Ushelisheli, na imetoa uungaji mkono mkubwa katika kuboresha maisha ya watu na kufikia malengo ya maendeleo ya nchi hiyo," ameongeza.
Herminie amesema Ushelisheli inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inapenda kuimarisha ushirikiano ndani ya mifumokazi ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika ili kuendelea kuzidisha uhusiano wa pande mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



