Eneo la Xiong'an, China lashuhudia ufufukaji wa ajabu wa hali ya ikolojia ya Ziwa Baiyangdian

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 26, 2026
Eneo la Xiong'an, China lashuhudia ufufukaji wa ajabu wa hali ya ikolojia ya Ziwa Baiyangdian
Picha iliyopigwa Juni 24, 2026 ikionyesha mandhari ya Ziwa Baiyangdian katika Eneo Jipya la Xiong'an, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (Xinhua/Mu Yu)

Tangu kuanzishwa kwa Eneo Jipya la Xiong'an nchini China, Ziwa Baiyangdian kwenye eneo hilo limepitia juhudi kubwa za urejeshaji wa hali ya ikolojia, ikiwa ni pamoja na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, uchimbaji mifereji, ujazaji maji kwa ajili ya hali ya ikolojia na urejeshaji wa ardhi oevu. Ubora wa maji ya ziwa hilo ulifikia Daraja la III kwa mujibu wa vigezo vya ubora wa maji ya ardhi vya China mwaka 2021 na umebaki tulivu katika kiwango hicho kwa miaka mitano mfululizo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha