Lugha Nyingine
Hafla ya kupandisha bendera na kuandaa tafrija vyafanyika kuadhimisha miaka 29 tangu Hong Kong kurudi China

Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) imefanya hafla ya kupandisha bendera kwa kusherehekea miaka 29 tangu Hong Kong kurudi China huko Hong Kong, kusini mwa China, Julai 1, 2026. (Xinhua/Zhu Wei)
HONG KONG – Jana Jumatano Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) imefanya hafla ya kupandisha bendera na kuandaa tafrija kusherehekea miaka 29 tangu Hong Kong kurudi China.
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China Leung Chun-ying, Ofisa Mtendaji Mkuu wa HKSAR John Lee, na Zhou Ji, na mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Serikali ya Kuu ya China katika Hong Kong, walishiriki kwenye hafla hiyo ya kupandisha bendera kwenye Uwanja wa Dhahabu wa Bauhinia Jumatano asubuhi.
Kufuatia hafla hiyo, tafrija ilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano na Maonyesho cha Hong Kong.
Kwenye tafrija hiyo, Lai Ka-ying, mwanaanga wa kwanza wa Hong Kong, alitoa hotuba kwa njia ya video kutoka kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China.
Lai amesema ni heshima kubwa kwake kuonyesha bendera ya HKSAR kwenye kituo hicho cha anga ya juu ili kutoa shukrani za dhati kwa nchi na kuitakia kila la kheri Hong Kong.
"Ninaitakia kwa dhati HKSAR ustawi na utulivu zaidi chini ya uangalizi na uungaji mkono wa nchi yetu. Tuungane mikono na kufanya juhudi za pamoja kwa ajili ya mustakabali mzuri zaidi wa nchi yetu na Hong Kong," amesema.
Katika hotuba yake kwenye tafrija, John Lee amesema siku zote anaiongoza serikali ya HKSAR katika kuandaa mpango wa kwanza wa miaka mitano wa Hong Kong, na kazi ya kukusanya maoni na mapendekezo ya umma tayari imeanza.
"Hong Kong itachukua fursa zinazoletwa na maendeleo ya nchi, na kutumia nguvu zake bora za kuunganishwa na China Bara na dunia, vilevile matarajio yake ya kimataifa kwa kuhimiza maendeleo ya uchumi na kuuwezesha wakazi wa Hong Kong kunufaika vizuri zaidi matokeo ya maendeleo," Lee amesema.
Lee alisema, Siku hiyo ya Jumatano pia ni siku ya maadhimisho ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China, na ustawi na neema kwa nchi daima vimekuwa msaada mkubwa kwa Hong Kong.
Asubuhi ya siku hiyo ya Jumatano, Ofisi ya Mawasiliano ya Serikali Kuu ya China katika Hong Kong, Ofisi ya Kulinda Usalama wa Nchi ya Serikali Kuu ya China katika HKSAR, na Ofisi ya Wajumbe Maalumu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China katika HKSAR, pia zilifanya hafla za kupandisha bendera.

Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) ikifanya tafrija kusherehekea maadhimisho ya miaka 29 tangu Hong Kong kurudi China huko Hong Kong, kusini mwa China, Julai 1, 2026. (Xinhua/Chen Duo)

Hafla ya kupandisha bendera ikifanywa na serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) kusherehekea miaka 29 tangu Hong Kong kurudi China, kusini mwa China, Julai 1, 2026. (Xinhua/Zhu Wei)

Kwenye hafla ya kupandisha bendera iliyofanywa na HKSAR kusherehekea miaka 29 tangu Hong Kong kurudi China, helikopita zilizoruka mbinguni zikionesha bendera ya taifa na bendera ya serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, kusini mwa China, Julai 1, 2026. (Xinhua/Zhu Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



