Maandamano ya kupinga uhamiaji ya Afrika Kusini yawa ya amani kwa kiasi kikubwa chini ya hatua kali za ulinzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 02, 2026

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

JOHANNESBURG - Afrika Kusini imeshuhudia maandamano ya kitaifa dhidi ya uhamiaji haramu juzi Jumanne, huku maelfu ya waandamanaji wakiandamana katika miji mikubwa chini ya ulinzi ulioimarishwa.

Mamlaka zimesema mikusanyiko mingi ilikuwa ya amani, ingawa matukio machache ya vurugu na uporaji yameripotiwa.

Maandamano hayo yaliyoratibiwa, yaliyoandaliwa na Operesheni Dudula, March and March, na makundi mengine vya kupinga uhamiaji, yalifuata amri ya mwisho iliyotolewa na waandaaji wakiiweka Juni 30 kuwa tarehe ya mwisho kwa wahamiaji wasio na vibali kuondoka nchini humo.

Waandamanaji wametoa wito wa udhibiti mkali wa mipaka, hatua kali za kusimamia utekelezaji wa sheria za uhamiaji na kufukuzwa haraka kwa wahamiaji wasio na vibali.

Mamlaka zilikuwa zimetuma maelfu ya maafisa wa polisi kote nchini kabla ya maandamano hayo, wakiungwa mkono na vitengo maalum vya Polisi wa Kusimamia Utaratibu wa Umma, huku jeshi likiwa katika hali ya utayari.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Gauteng, Tommy Mthombeni, alisema Jumatatu kwamba maafisa takriban 13,000 wa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini, maafisa zaidi ya 10,000 wa polisi wa miji, walinzi wa trafiki wapatao 8,000 na wafanyakazi zaidi ya 217,000 wa usalama binafsi walikuwa wamehamasishwa kote jimboni humo kufuatilia maandamano na kudumisha utulivu wa umma.

Maandamano mengi yalifanyika kwa amani chini ya uwepo mkubwa wa polisi, ingawa mamlaka zimeripoti matukio kadhaa ya jinai. Katika Jimbo la KwaZulu-Natal, polisi waliwakamata washukiwa wasiopungua 10 kwa uporaji na kujaribu kupora mjini Durban na maeneo ya jirani.

Katika Jimbo la Gauteng, watu wawili walijeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi huko Hillbrow, Johannesburg, kwenye maandamano. Msemaji wa polisi wa jimbo, Brenda Muridili, amesema washukiwa waliwafyatulia risasi waathiriwa kwenye maandamano dhidi ya raia wa kigeni wasio na vibali.

Baadaye siku hiyo ya Jumanne, serikali ilikaribisha mwenendo wa amani wa maandamano hayo ya kitaifa na kuwashukuru Waafrika Kusini kwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa kuwajibika. Pia iliwapongeza viongozi wa jamii, mashirika ya kiraia, viongozi wa kidini, waandaaji wa maandamano na vyombo vya kusimamia utekelezaji wa sheria kwa kusaidia kuhakikisha kwamba mikusanyiko mingi ilikamilika bila vurugu kubwa.

Serikali imesisitiza kwamba mtu yeyote anayehusika na vurugu, uporaji au vitendo vingine vya uhalifu kwenye maandamano atakamatwa na kushtakiwa.

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

Waandamanaji wakiandamana kwenye maandamano dhidi ya uhamiaji haramu jijini Durban, Afrika Kusini, Juni 30, 2026. (Picha na Mbuthi Msweli/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha