Reli ya Qinghai-Xizang yaleta mabadiliko makubwa kwenye uwanda wa juu wa theluji wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 02, 2026

Picha hii ya kuunganisha ikimuonesha Tatso (kulia) na rafiki yake wakifurahia kwenye sehemu ya ujenzi wa Reli ya Qinghai-Xizang karibu na nyumbani kwao katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Machi 30, 2005 (hapo juu, picha na mwandishi wa habari picha wa Xinhua Chogo), na Tatso (kulia wa kwanza) na binti zake watatu wakipiga picha kando ya Reli ya Qinghai-Xizang katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026 (hapo chini, picha na mwandishi wa habari picha wa Xinhua Jiang Fan).

Miaka ishirini na moja iliyopita, wakati ujenzi wa Reli ya Qinghai-Xizang ulipokuwa ukiendelea, mwandishi wa habari picha wa Shirika la Habari la China, Xinhua Bw.Chogo alipopiga picha alinasa wasichana wawili wenye tabasamu angavu usoni waliokaa kando ya reli kwenye sehemu ya ujenzi wa reli katika Wilaya ya Damxung, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China Machi 30, 2005.

Hivi sasa, mmoja wa wasichana hao, Tatso, amekuwa mama wa watoto watatu, alipokutana tena na waandishi wa habari picha wa Xinhua alizungumzia mabadiliko makubwa yaliyotokea katika Uwanda wa Juu wa theluji kutokana na njia hiyo ya reli.

"Ninapotazama treni zikipita hapa kila siku, inanifanya nibaini kwamba miaka ishirini na moja imepita kwa kufumba na kufumbua macho." Tatso amesema.

Tangu Reli ya Qinghai-Xizang ilipozinduliwa rasmi kuanzia tarehe Mosi Julai, 2006, historia ya muda mrefu ya Xizang ya kutokuwa na njia ya reli ilikomeshwa kabisa, hivi sasa jumla ya bidhaa zinazosafirishwa kwa njia ya reli kuingia na kutoka Xizang imezidi tani milioni 100, na idadi ya safari za abiria imezidi milioni 41.

Treni ikipita katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Katika miongo hiyo miwili iliyopita, Reli ya Qinghai-Xizang, ambayo ni njia kuu ya usafirishaji, imekuwa ikiboresha siku hadi siku maisha ya watu wanaoishi kwenye uwanda wa juu.

Miaka ishirini iliyopita, familia ya Tatso ilikuwa na pikipiki moja nyumbani, na mapato yao yalidumishwa kwa ufugaji tu wa mifugo. Hivi sasa, ikitegemea ufugaji wa mifugo na usafirishaji wa mizigo, familia hiyo inamiliki malori matatu, mtambo wa kupakia mizigo, magari mawili ya kibinafsi na pikipiki mbili, na ng’ombe wa yaki zaidi ya 50.

"Aina zote za nguo na mahitaji ya kila siku vinaweza kununuliwa." Tatso amesema akiwa ameshikilia mabinti zake. Mbele ya kamera ya waandishi wa habari picha wa Xinhua, Tatso amepiga picha na mabinti zake, ambao walikuwa wamevaa mavazi mazuri na ya kimitindo, yakitofautiana sana na nguo za Tatso zilizokuwa na madoa ya mafuta na zilizochakaa kwenye picha ya zamani.

"Sasa nina matamanio mawili. Kwanza, natumai watoto wangu watatu wanaweza kusoma kwa bidii na kukua kwa afya njema. Pili, nitakapopata muda katika siku za baadaye, nitawapeleka watoto wangu kwa kupanda treni kutembelea mji mkuu wa Beijing." amesema Tatso.

Tatso akiwa na watoto wake ndani ya gari lake, huku treni ikionekana nyuma, katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026. (Xinhua/Jiang Fan)

Tatso (wa pili kulia) na binti zake watatu wakifurahia kwenye eneo la malisho ya mifugo katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Tatso (wa kwanza kulia) na binti zake watatu wakipiga picha mbele ya nyumba yao pembeni ya Reli ya Qinghai-Xizang katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Tatso akitembea kwenye eneo la malisho ya mifugo mbele ya nyumba yake katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Tatso (wa pili kushoto) na familia yake wakipiga picha pamoja kwenye ua wa nyumba yao katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Juni 21, 2026. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Picha iliyopigwa Juni 21, 2026 ikionyesha nyumba ya Tatso katika Wilaya ya Damxung ya Lhasa, Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Tenzin Nyida)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha