Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema China na Marekani zinapaswa kushikilia kujenga uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati

(CRI Online) Julai 03, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema, China na Marekani zinapaswa kuondoa usumbufu na vizuizi, na kushikilia mwelekeo sahihi wa kujenga uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati kati ya pande mbili.

Wang ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio siku ya Jumanne, akibainisha kuwa mwezi Mei mwaka huu, Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump walifikia mlolongo wa makubaliano ya pamoja hapa Beijing, ikiwa ni pamoja na kujenga uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati kati ya pande hizo mbili, ambao umetoa mwongozo wa kimkakati na kuweka mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili katika kipindi cha miaka mitatu ijayo na zaidi.

Wang amesisitiza kuwa pande zote mbili zinapaswa kudumisha moyo wa usawa, kuheshimiana na kunufaishana, na kutafsiri makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu hao wawili wa nchi katika sera maalum na hatua za kivitendo.

Kwa upande wa suala la Taiwan Wang amesema lina athari kubwa, hivyo ameihimiza Marekani kushughulikia masuala yanayohusiana na Taiwan kwa busara zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha