Lugha Nyingine
Kenya yaongeza kasi ya kuwarejesha nyumbani raia wake walioko Afrika Kusini
Kenya imetangaza kuwarejesha nyumbani raia wake 151 waliokuwa Afrika Kusini kutokana na mvutano unaoongezeka dhidi ya wahamiaji nchini humo.
Akitoa tangazo hilo jana Alhamisi, Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi alisema jumla ya raia 240 wa Kenya wanaohitaji msaada wamejiandikisha kwenye Ubalozi Mkuu wa Kenya huko Pretoria. Mudavadi alisema ubalozi huo kwa sasa unatoa makazi salama ya muda, ikiwa ni pamoja na malazi ya hoteli, chakula, na vifaa vingine muhimu vya misaada, pamoja na usaidizi maalum kwa watu walio katika mazingira magumu.
Mudavadi, ambaye alifanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mahusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, alibainisha kuwa wengi wa Wakenya 27,000 wanaokadiriwa kuishi Afrika Kusini wanaendelea kutoa michango muhimu kwa ustawi wa mataifa yote mawili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



