Ofisa wa Africa CDC asema mlipuko wa Ebola umefikia katika “hali mbaya sana” nchini DRC

(CRI Online) Julai 03, 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Jean Kaseya Alhamisi amesema, mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umefikia katika "hali mbaya sana", ambapo watu zaidi ya 400 wameripotiwa kufariki.

Amesema ikilinganishwa na milipuko ya awali ya Ebola nchini DRC na mlipuko wa Ebola wa Afrika Magharibi kwenye hatua kama hii, mlipuko huu wa sasa umerekodi kasi kubwa ya ongezeko la wagonjwa na vifo. Serikali inachukua hatua sahihi za kuzuia kuenea kwa homa ya Ebola na kutokomeza janga hilo.

Kwa mujibu wa serikali, hadi kufikia Jumanne watu 1,406 nchini DRC wamethibitishwa kuambukizwa homa ya Ebola, na 438 kati yao wamefariki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha