Lugha Nyingine
Rais wa Uganda aunga mkono viza moja ya Afrika Mashariki kwa ajili ya AFCON 2027
(CRI Online) Julai 03, 2026
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha pendekezo la kuanzisha viza moja ya kuingia Afrika Mashariki kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) la mwaka 2027, ambalo Uganda itaandaa pamoja na Kenya na Tanzania.
Rais Museveni amewaagiza maafisa kuanza mashauriano na wenzao wa Kenya na Tanzania ili kuendeleza pendekezo hilo kabla ya mashindano. Viza iliyopendekezwa itawaruhusu mashabiki wa mpira wa miguu, watalii, maafisa wa mechi na timu shiriki kusafiri kwa uhuru katika nchi tatu wenyeji kwa muda wa hadi miezi minne bila kuhitaji vibali tofauti vya kuingia kwenye nchi hizo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



