Vifo vya watu vinavyotokana na Ebola vyakaribia 500 nchini DRC na maambukizi yanayoendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 06, 2026

Picha hii ikionyesha familia kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Picha hii ikionyesha familia kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

KINSHASA - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeripoti watu 1,528 walioithibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Ebola, watu 492 kati yao wamefariki dunia kutokana na mlipuko huo unaoendelea kuenea nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya hali iliyotolewa Jumamosi na mamlaka za afya ya umma za DRC, wagonjwa jumla ya 239 wamepona, hivi sasa wagonjwa 628 waliothibitishwa virusi wako katika karantini au hospitalini. Mamlaka pia zimegundua watu 185 walioshukiwa kuambukizwa virusi.

Ripoti hiyo imesema idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi kila wiki inaendelea kuongezeka, huku rekodi za mlipuko wa ugonjwa huo za wiki ya 25 na 26 zikionyesha viwango vya juu zaidi hadi sasa, kila wiki moja ikizidi wagonjwa 300, hali ambayo inaonyesha maambukizi yanayoendelea kwenye maeneo ya wakazi.

Ripoti hiyo imetaja changamoto kadhaa kubwa, ikiwa ni pamoja na maeneo ya wakazi kupinga uchukuaji wa sampuli baada ya kutokea kwa vifo vya watu, uwezo mdogo katika vituo vya matibabu ya Ebola, hasa katika jimbo la mashariki la Kivu Kaskazini, ufuatiliaji mdogo wa watu waliokutana na kugusana na wagonjwa au watu wanaoshukuiwa kuambukizwa, kuchelewa kwa upimaji wa maabara, uhaba wa zana na vifaa vya kinga na matibabu ya maambukizi, hali isiyo ya usalama na vizuizi vya usafiri katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na maambukizi ya ugonjwa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) ilisema Alhamisi kwamba majaribio ya hospitalini yameanza kutumika kwa wagonjwa nchini DRC ili kutathmini uwezekano wa matibabu ya ugonjwa huo wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo, ambavyo hadi kufikia sasa havina chanjo iliyoidhinishwa au matibabu maalum. 

Mwanamke akitundika nguo kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Mwanamke akitundika nguo kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Mwanamke na mtoto wakionekana kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Mwanamke na mtoto wakionekana kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Watoto wawili wakionekana kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Watoto wawili wakionekana kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Jamaa akitumia cherehani kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Jamaa akitumia cherehani kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Mwanamke akimsaidia mwanamke mwingine kusuka nywele kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

Mwanamke akimsaidia mwanamke mwingine kusuka nywele kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao karibu na Bunia, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 4, 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha