Lugha Nyingine
China na Russia zaanza kufanya mazoezi ya pamoja ya vikosi vya majini (5)
QINGDAO - China na Russia zimeanza kufanya mazoezi ya "Joint Sea-2026" kwenye bandari ya kijeshi ya Qingdao katika Mkoa wa Shandong mashariki mwa China, ambapo makao makuu ya pamoja yameanzishwa, yakiundwa na vikosi vya majeshi ya majini ya nchi hizo mbili.
Mazoezi hayo yaliyoanza jana Jumatatu yatafanywa katika vipindi vitatu: mkusanyiko wa vikosi, mpangilio kwenye bandari, na mazoezi ya kupigana vita baharini. Mkusanyiko wa vikosi ulikamilishwa juzi Jumapili.
Baada ya kufanyika hafla ya ufunguzi, vikosi hivyo viwili vya majini vilifanya mazoezi ya uongozi na uratibu wa kimkakati. Makao makuu ya pamoja yalifanya majadiliano ya kina juu ya mambo muhimu ya mazoezi ya kupigana vita baharini.
Kwa hatua inayofuata, manowari zinazoshiriki zitaelekea eneo la baharini karibu na Qingdao kufanya mazoezi ya upelelezi kwa pamoja, ulinzi wa anga na makombora, pamoja na mazoezi katika matumizi halisi ya silaha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




