Lugha Nyingine
Xi atoa wito wa kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China kupitia uvumbuzi wa sayansi na teknolojia (4)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kuharakishwa kwa juhudi za kutimiza kujitegemea na kuwa na nguvu kwa kiwango cha juu katika sayansi na teknolojia, na kutumia kikamilifu uvumbuzi wa sayansi na teknolojia kwa kutoa nguzo na msukumo kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ameyasema hayo jana Jumatano kwenye mkutano uliofanyika mjini Beijing, ambao walikusanyika pamoja wajumbe wa mkutano wa kitaifa wa tuzo za sayansi na teknolojia, mikutano ya wajumbe wa Taasisi kuu ya Sayansi ya China (CAS) na Taasisi kuu ya Uhandisi ya China (CAE), na mkutano wa 11 wa kitaifa wa Shirika la Sayansi na Teknolojia la China.
Amesema kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) ni kipindi muhimu kwa kukabiliana na changamoto ngumu katika kujenga nguvu ya nchi ya sayansi na teknolojia.
"Lazima tutumie fursa ya kihistoria, tukabiliane na changamoto za zama tulizo nazo, tuharakishe juhudi za kufikia kujitegemea na kuwa na nguvu kwa kiwango cha juu katika sayansi na teknolojia, na tusonge mbele kwa hatua madhubuti kuelekea lengo la mwaka 2035 la kufanikisha kujenga nchi kuwa nchi yenye nguvu kubwa katika sayansi na teknolojia," amesema.
Kwenye mkutano huo, Xi alikabidhi tuzo ya juu ya sayansi na teknolojia ya China ya mwaka 2025 kwa Chen Liquan, mtafiti katika Taasisi ya Fizikia katika CAS ambaye pia ni mtaalamu mkuu wa CAE, na Ben De, mtafiti katika kampuni ya Kundi la Teknolojia ya Elektroniki la China ambaye pia ni mtaalamu mkuu wa CAE. Baada ya kuwakabidhi wanasayansi hao wawili nishani na vyeti, Xi alishikana nao mikono na kuwapongeza.
Xi na viongozi wengine wa Chama na serikali, pamoja na washindi hao wawili wa tuzo ya juu, walikabidhi vyeti kwa wawakilishi wa wapokeaji wa tuzo nyingine.
Mbali na wapokeaji hao wawili wa tuzo ya juu, wataalamu tisa wa kigeni walitunukiwa Tuzo ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Sayansi na Teknolojia ya China.
Xi amesema hivi sasa China inaharakisha mpito wake kutoka kuwa mshiriki na mchangiaji hadi kuwa mtangulizi na kiongozi katika sayansi na teknolojia za dunia nzima, na imekuwa moja ya nchi zenye uwezo wa uvumbuzi unaokua kwa kasi zaidi.
Lakini Xi pia amesema pia China bado ina mapengo katika uwezo wa uvumbuzi wa awali, muundo usio na uwiano wa vipaji, na matumizi yasiyo na ufanisi ya uwekezaji wa sayansi na teknolojia, yote hayo yanahitaji ufuatiliaji na utatuzi makini sana.
Amesisitiza kwamba raundi mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na mabadiliko makubwa ya viwanda inabadilisha kwa kina njia za binadamu katika kuzalisha bidhaa na kuishi maisha, pamoja na muundo wa maendeleo ya dunia nzima.
Xi pia ametoa wito wa kukamilisha mfumo wa ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu na kujenga mfumo wa mambo ya fedha unaoendana na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




