Vikosi vya majeshi ya China na Russia vyafanya mazoezi ya kupigana vita kwa silaha halisi baharini (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2026
Vikosi vya majeshi ya China na Russia vyafanya mazoezi ya kupigana vita kwa silaha halisi baharini
Picha hii iliyopigwa Julai 9, 2026 ikionyesha manowari za vikosi vya majini vya majeshi ya China na Russia zikiendeshwa kwa mpangilio maalum kwenye mazoezi ya kupigana vita baharini katika mazoezi ya "Joint Sea-2026". (Xinhua/Li Bingxuan)

Manowari za vikosi vya majini vya majeshi ya China na Russia jana Alhamisi zilianza kufanya mazoezi ya kupigana vita kwa silaha halisi baharini katika maeneo yaliyotengwa karibu na mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China.

Mazoezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya "Joint Sea-2026", ambayo yalianza Jumatatu wiki hii kwa vipindi vitatu: kukusanyika kwa vikosi, mipango ya bandarini na mazoezi ya kupigana vita baharini.

Kwa mujibu wa mpango wa mazoezi hayo, kipindi cha kupigana vita baharini kinahusisha mazoezi ya upelelezi wa pamoja, ulinzi wa anga na mapambano dhidi ya makombora, na mazoezi ya kufanya ushirikiano katika utafutaji na uokoaji kwa kutumia nyambizi.

Kabla ya mazoezi ya kupigana vita baharini, askari wa China na Russia wanaoshiriki walifanya mfululizo wa shughuli za mawasiliano kwenye nchi kavu, ikiwa ni pamoja na kutembeleana kwenye manowari za kila upande.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha