Eneo la Maendeleo ya Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya Juu la Jinan, China lasukuma mbele mfumo wa kisasa wa viwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2026
Eneo la Maendeleo ya Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya Juu la Jinan, China lasukuma mbele mfumo wa kisasa wa viwanda
Mfanyakazi akirekebisha roboti kwenye Kampuni ya Mambo ya Roboti za AI ya Shandong Yobotics katika Eneo la Maendeleo ya Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya Juu la Jinan Mkoani Shandong, mashariki mwa China, Julai 11, 2026. (Xinhua/Guo Xulei)

Eneo la Maendeleo ya Viwanda vya Teknolojia ya Hali ya Juu la Jinan katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, ni moja ya maeneo ya kwanza ya teknolojia ya hali ya juu ya ngazi ya kitaifa ya China.

Katika miaka ya hivi karibuni, eneo hilo limeendelea kuboresha mazingira yake ya biashara na kuharakisha kasi ya kujenga mfumo wa kisasa wa viwanda. Si tu limeimarisha viwanda vyake vitatu muhimu vya teknolojia za kupashana habari za kizazi kipya, vifaa janja na dawa za binadamu, lakini pia limepanga mapema kabla ya muda kuendeleza viwanda vya siku za baadaye ikiwa ni pamoja na AI, uchumi wa anga ya chini na biolojia ya sintetiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha