Lugha Nyingine
China na Russia zamaliza mazoezi ya pamoja ya vikosi vya majini (7)
![]() |
| Askari wa Kikosi cha Majini cha China wakifanya mazoezi ya kufyatua silaha halisi moja kwa moja katika mazoezi ya kupigana vita kwenye bahari katika mazoezi ya "Joint Sea-2026" ya vikosi vya majini vya China na Russia, Julai 9, 2026.(Picha na Li Fengxiang/Xinhua) |
QINGDAO - Mazoezi ya "Joint Sea-2026" kati ya China na Russia yamemalizika kwenye bandari ya kijeshi ya Qingdao, Mkoa wa Shandong mashariki mwa China jana Jumatatu, huku majukumu yote ya mazoezi yaliyopangwa yakimalizika.
Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, baadhi ya vikosi vinavyoshiriki vya nchi hizo mbili vimesafiri kwenda Pasifiki kufanya doria za pamoja.
Vikosi hivyo viwili vya majini vimetuma manowari 10, ikiwa ni pamoja na manowari zinazoendeshwa kwenye maji, nyambizi, manowari za kubeba ndege na za uungaji mkono, lengo kuu la mazoezi hayo ni "kukabiliana kwa pamoja na hatari za usalama wa baharini."
Katika kipindi cha mazoezi ya kupigana vita kwenye bahari, pande hizo mbili zilifanya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano ya mezani kuhusu hali ya kupigana vita, kutembelea kwenye manowari, kufanya kongamano kuhusu taalamu, na kufanya tamasha la muziki na dansi, pamoja na mechi za mpira wa kikapu.
Kwenye bahari, walifanya mazoezi ya kupigana vita na kufyatua silaha halisi moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na upelelezi wa pamoja, ulinzi wa anga na mapambano dhidi ya makombora, kuzuia mashambulizi dhidi ya eneo la majini, na kufanya uokoaji wa pamoja kwa kutumia nyambizi.
Mwongozaji mkuu wa mazoezi hayo ya pamoja amesema, mazoezi hayo yaliigilizia mazingira halisi ya mapigano ya baharini na angani, na kuonesha mwelekeo wa kuwa na nguvu kubwa ya kupigana vita katika mazingira halisi.
Mwongozaji mkuu huyo amesema pia kuwa, mazoezi hayo ya pamoja yameongeza zaidi hali ya kuaminiana kimkakati kwa majeshi hayo mawili, kuimarisha urafiki wa muda mrefu na kuongeza uwezo wao wa kukabiliana kwa pamoja na misukosuko ya baharini.
Mazoezi hayo ya "Joint Sea-2026" yalianzishwa Tarehe 6 Julai, ni mazoezi ya 12 katika mfululizo wake kuanzia mwaka 2012.
Zheng Hong, mtafiti wa Taasisi ya Utafiti ya Jeshi la Majini la China amesema mazoezi hayo ya pamoja yana umuhimu kwa hali ilivyo sasa ya kulinda amani na utulivu wa kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




