Xi asisitiza kujenga upya miji ya kiwango cha juu katika ziara ya ukaguzi mjini Shanghai (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2026
Xi asisitiza kujenga upya miji ya kiwango cha juu katika ziara ya ukaguzi mjini Shanghai
Rais wa China Xi Jinping, akizungumza na wakazi, maofisa wa mitaa na wafanyakazi wa jumuiya ya wakazi kwenye sehemu moja ya makazi katika Eneo la Huangpu la Shanghai, mashariki mwa China, Julai 15, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

SHANGHAI - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa wito wa kusukuma mbele kazi ya kujenga upya miji ya kiwango cha juu jana Jumatano wakati wa ziara ya ukaguzi mjini Shanghai.

Amesisitiza kupokea kikamilifu wazo la maendeleo ya miji ya kutoa kipaumbele kwa watu.

"Mipango ya kujenga upya miji inapaswa kuhimizwa kwa pande zote, kwa makini zaidi na kwa njia yenye ufanisi, ili kuongeza hisia za watu za kuridhika, kuona furaha na usalama hatua kwa hatua," amesema.

Katika Eneo la Huangpu, Xi alitembelea sehemu moja ya makazi, ambapo majengo manne yaliyojengwa miaka ya 1950 yamefanyiwa ukarabati na kupandishwa ngazi ya ujenzi, na hivyo kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya maisha ya wakazi.

Amesisitiza kwamba Kamati Kuu ya Chama inatilia maanani sana maendeleo ya miji na imeahidi kujenga miji ya mambo ya kisasa kwa ajili ya watu, na kazi za ukarabati wa sehemu za makazi za zamani ni sehemu muhimu ya juhudi hizo.

Katika nyumba ya mkazi mmoja mstaafu, Xi alitazama kwa makini hali ya nyumba ya kuishi na kusema kwamba CPC inautumikia umma kwa moyo wote, na ni pale tu watu wanapoishi kwa amani na kuridhika ndipo Chama na serikali vitakuwa na uhakika. Amewatumai wastaafu wanaweza kuishi vizuri zaidi katika maisha yao ya ustaafu, na familia zao zitakuwa na maisha bora zaidi.

Kisha Xi alitembelea kibanda cha uuzaji wa mazao freshi kwenye sehemu ya makazi, ambapo alikagua utoaji wa matunda na mboga za majani. Amesisitiza umuhimu wa kuboresha usimamizi wa sehemu za makazi na kukamilisha majengo husika na kuongeza urahisi wa maisha ya wakazi katika sehemu za makazi.

Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Xi amesisitiza kwamba hivi sasa China iko katika kipindi muhimu cha kuzuia mafuriko. Amezihimiza sehemu mbalimbali nchini kujiandaa kwa kukabiliana na uwezekano wa kutokea matukio mabaya zaidi na hali mbaya kupitiliza, kufuatilia kwa karibu mvua, hali ya mafuriko na mwelekeo wa kimbunga, kufanya ukaguzi wa kina na makini ili kugundua hatari zinazoweza kutokea, na kufanya juhudi kubwa zenye ufanisi katika kuzuia na kudhibiti mafuriko, kukabiliana na hali ya dharura na kutoa misaada kwa walioathiriwa, na kuhakikisha kwa ufanisi usalama wa maisha na mali za watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha