Lugha Nyingine
Mji wa Chengdu waendeleza mfumo kamili wa kiikoloia wa roboti (4)
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Chengdu katika Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China umeongeza juhudi za kujenga viwanda vyake vya teknolojia ya AI na mambo ya roboti, na kuimarisha mkusanyiko wa viwanda na kukuza mfumo ikolojia jumuishi wa mambo ya roboti.
Ili kukidhi vizuri zaidi mahitaji ya sekta mbalimbali, kituo cha mafunzo ya teknolojia na uvumbuzi wa roboti cha Maabara ya Tianfu Jiangxi mjini Chengdu kimejenga eneo maalum la mafunzo ya roboti la mfano wa mazingira ya hali ya maisha halisi ya watu. Kituo hicho pia kimeanzisha jukwaa la data linaloweza kutoa seti za data mfufulizo kuhusu mazingira ya hali mbalimbali, na kusaidia roboti kutumia kile zilichojifunza katika matumizi ya hali na mazingira halisi.
Baada ya kupata mafunzo ya kutosha, roboti ziko tayari kwa matumizi ya kibiashara. Mapema mwezi huu, duka la roboti za AI la ROBO+ lilifunguliwa Chengdu. Duka hilo linaunganisha kazi yake ya uuzaji wa rejareja na wateja kujaribu huduma hiyo, likionyesha uvumbuzi wa AI na mambo ya roboti kutoka sehemu mbalimbali nchini China na kuifanya teknolojia mpya ikaribie watu zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




