Lugha Nyingine
Uokoaji waendelea baada ya maporomoko ya mlima kutokea Chongqing, China (4)
Tukio la kuporomoka kwa mlima lililosababishwa na mvua lilitokea majira ya 3:08 asubuhi siku ya Ijumaa iliyopita katika Wilaya Inayojiendesha ya Makabila ya Wamiao na Watujia ya Pengshui, huko Chongqing, kusini magharibi mwa China, ambapo majengo ya makazi zaidi ya 10 yalifunikwa papo hapo, na baadhi ya wakazi wamenaswa na wengine bado hawajajulikana walipo.
China ilianzisha mpango wa kitaifa wa ngazi ya pili wa kukabiliana na maafa ya dharura ya kijiolojia. Vikosi mbalimbali vya uokoaji vikiwemo vya kukabiliana na hali ya dharura, udhibiti wa moto na usalama wa umma vilikimbilia eneo la tukio na kuanzisha operesheni za kufanya utafutaji na uokoaji kwa pande zote, wakati huohuo wakazi wa huko pia wamejitolea kushiriki katika juhudi hizo za uokoaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




