Rais wa Tanzania apongeza mchango wa kampuni za China katika maendeleo ya miundombinu (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2026
Rais wa Tanzania apongeza mchango wa kampuni za China katika maendeleo ya miundombinu
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (wa tano, kulia) akiongoza hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa sehemu ya sita ya Reli ya SGR inayojengwa na kampuni ya China, inayounganisha mikoa ya Tabora na Kigoma, katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania, Julai 20, 2026. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

DAR ES SALAAM - Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezishukuru kampuni za China kwa mchango wao katika juhudi za maendeleo za nchi hiyo zinazolenga kunufaisha watu wake.

Rais Samia alitoa kauli hiyo jana Jumatatu baada ya kuongoza hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa sehemu ya sita ya Reli ya SGR inayojengwa na kampuni ya China, inayounganisha mikoa ya Tabora na Kigoma.

Mradi huo unajengwa kwa ubia kati ya Shirika la Ujenzi wa Reli la China (CRCC) na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China (CCECC).

Rais Samia amesisitiza mchango muhimu ambao kampuni za China zinatoa katika kuendeleza miundombinu ya usafiri na uchukuzi ya Tanzania, wakati huohuo pia amesisitiza matokeo chanya yanayotarajiwa kutoka kwenye reli hiyo itakapokamilika, ikiwemo kufupishwa kwa muda wa kusafiri, kupungua kwa gharama za usafiri, na uundaji wa ajira.

"Mradi huu unaonyesha dhamira yetu katika kupanua miundombinu ya kisasa ya usafiri ili kufungua biashara, kupunguza gharama na kuunganisha watu na biashara zetu na masoko ya ndani na kimataifa," amesema.

Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Makame Mbarawa amesema upanuzi wa reli hiyo ya SGR ni sehemu ya mkakati mpana zaidi wa kufungamanisha reli, bandari na usafiri wa anga, na kuiweka Tanzania katika nafasi ya kuwa kituo cha usafirishaji cha kikanda chenye uwezo wa kushindana.

Zhang Junle, naibu meneja mkuu wa CCECC, amesema reli hiyo ya SGR ya Tanzania ni mradi mkuu wa uti wa mgongo wa Ushoroba wa Maendeleo wa Kati katika Afrika Mashariki.

Amesema mradi huo utakapokamilika, utachochea maendeleo yaliyoratibiwa ya sekta kama vile za kilimo, biashara, na utalii kando ya njia hiyo, na kuingiza kasi kubwa katika mafungamano ya kiuchumi ya kikanda katika Afrika Mashariki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha