Jukwaa la Maendeleo ya Kidijitali ya Njia ya Hariri la Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 lafunguliwa Xi'an, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2026
Jukwaa la Maendeleo ya Kidijitali ya Njia ya Hariri la Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 lafunguliwa Xi'an, China
Washiriki wakionekana kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Kidijitali ya Njia ya Hariri la Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zou Jingyi)

Jukwaa la Maendeleo ya Kidijitali ya Njia ya Hariri la Mkutano wa Intaneti Duniani 2026 lenye kaulimbiu ya "Kukusanya Maarifa ya Njia ya Hariri, Kuanzisha Mustakabali wa Kidijitali -- Kujenga kwa Pamoja Jumuiya ya Nafasi ya Mtandao yenye Mustakabali wa Pamoja" limefunguliwa Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China jana Jumatano.

Jukwaa hilo limevutia washiriki takriban 800 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 50, pamoja na mashirika saba ya kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha