Tasnia ya nyuki weusi yaimarishwa katika Wilaya ya Raohe ya Kaskazini Mashariki mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2026
Tasnia ya nyuki weusi yaimarishwa katika Wilaya ya Raohe ya Kaskazini Mashariki mwa China
Yue Yun akionyesha nyuki weusi wa asali kwenye shamba la nyuki ndani ya hifadhi ya taifa ya mazingira ya asili katika Wilaya ya Raohe, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Julai 29, 2026. (Picha na Zhang Chunlei/Xinhua)

Yue Yun, mwanakijiji katika Kijiji cha Shuangsheng cha Wilaya ya Raohe katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, amekuwa akifanya biashara ya nyuki weusi kwa miaka 33.

Ili kupanua soko la asali inayozalishwa katika kijiji hicho, Wilaya ya Raohe katika miaka ya hivi karibuni imeanzisha kampuni ongozi, ambazo zimeanzisha ushirika kijijini hapo na pia kutoa mafunzo ya mbinu kwa wakulima wa nyuki, ili kuhakikisha ubora wa bidhaa za asali.

Hadi sasa, katika hifadhi ya taifa ya nyuki weusi wa kaskazini mashariki ya China, mashamba ya nyuki yapatayo 431 yameanzishwa na zaidi ya wafanyakazi 1,300 husika wameshiriki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha