Umeme uliosafirishwa kutoka kwa Njia ya usambazaji umeme ya Xinjiang-Chongqing wafikia kWh bilioni 30 (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2026
Umeme uliosafirishwa kutoka kwa Njia ya usambazaji umeme ya Xinjiang-Chongqing wafikia kWh bilioni 30
Mafundi wakifuatilia halijoto ya kituo kwenye kiwanja cha transfoma ya kupoza umeme ya kituo cha kupoza umeme cha Yubei cha mradi wa usafirishaji umeme wa volteji ya juu (UHV DC) wa ±800 kV wa Hami-Chongqing, kusini magharibi mwa China, Julai 30, 2026. (Xinhua/Huang Wei)

CHONGQING - Tangu kuanza kwa uendeshaji wa mradi wa usafirishaji wa umeme wa volteji ya juu (UHV DC) wa ±800 kV, mradi huo unaounganisha Hami ya Mkoa wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China na Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, sehemu ya Chongqing ya mradi huo imepokea kwa jumla zaidi ya kWh bilioni 30 za umeme, na kiwango cha juu zaidi cha usafirishaji wa umeme cha siku moja kilichorekodiwa kilifikia kWh milioni 145.

Njia hiyo kuu ya usafirishaji wa umeme kutoka kaskazini magharibi hadi kusini magharibi mwa China, imedumisha uendeshaji tulivu wakati wa kipindi cha matumizi makubwa zaidi ya umeme ya majira ya joto ya mwaka huu, ikitoa msukumo mkubwa kwa ajili ya utoaji wa umeme wa uhakika kwenye sehemu za makazi na maendeleo ya viwanda yenye sifa-bora. 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha