Hafla ya Kutangaza Kimataifa Utalii wa Kitamaduni wa Honghe, Yunnan 2026 yafanyika Beijing (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 03, 2026
Hafla ya Kutangaza Kimataifa Utalii wa Kitamaduni wa Honghe, Yunnan 2026 yafanyika Beijing
Shughuli ya kukusanya kaulimbiu za kuitangaza Honghe kwa mtandao mzima ikizinduliwa. (Picha na Xue Dan/People’s Daily Online)

Hafla ya Kutangaza Kimataifa Utalii wa Kitamaduni wa Honghe, Yunnan 2026 ilifanyika tarehe 31, Julai, kwenye Jengo la Vyombo Vipya vya Habari la People’s Daily mjini Beijing.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Utamaduni na Utalii ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wahani na Wayi la Honghe la Mkoa wa Yunnan, China, ilionesha rasilimali za utalii wa kukaa kwa muda mrefu na chapa zake za utalii wa kitamaduni kwa hadhira duniani.

Honghe ni eneo pekee la utalii wa kitamaduni duniani lenye urithi wa aina tatu uliothibitishwa kimataifa kwa wakati mmoja, yaani Urithi wa Kitamaduni wa Dunia, Urithi wa Mifumo ya Kilimo Yenye Umuhimu Duniani, na Urithi wa Miundo ya Umwagiliaji wa Dunia.

“Hao Zai” - ambayo inamaanisha “Hali ya kuwa na maisha mazuri” katika lahaja ya Yunnan – ni usemi wa kawaida wa watu wa Yunnan unaomaanisha maisha ya kufurahisha, na pia inabeba ahadi ya ukarimu kutoka eneo la Honghe.

Zhang Muxing, mjumbe wa kudumu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Eneo la Honghe na Naibu Mkuu wa Serikali ya Eneo la Honghe kwenye hafla hiyo alisema kuwa, mvuto wa eneo hilo unatokana na mazingira yake ya asili ya kupendeza na hazina zake nyingi za asili.

Alisema eneo hilo linajivunia tabianchi za aina mbalimbali, kuanzia mabonde ya mito hadi milima mirefu, ikiwa na kiwango cha kufunikwa na misitu kinachozidi 60% na uzalishaji mwingi wa bluberi, makomamanga, na mboga za kipekee za majani.

Kwenye hafla hiyo, wawakilishi wa Ofisi ya Utamaduni na Utalii ya Honghe na People’s Daily Online tawi la Yunnan walitia saini makubaliano ya mfumo wa ushirikiano juu ya kutangaza utalii wa kitamaduni. Chini ya makubaliano hayo, pande hizo mbili zitashirikiana kuongeza mvuto wa chapa ya utalii wa kitamaduni ya “Hao Zai Honghe”, na kuchochea maendeleo yenye sifa bora ya sekta ya utalii wa kitamaduni ya Honghe.

Tang Weihong, mjumbe wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya People’s Daily Online na naibu rais wa kampuni hiyo alihutubia hafla hiyo akisema, ushirikiano wa kina na Eneo la Honghe unawakilisha vitendo makini na mfano dhahiri wa namna chombo kikuu cha habari kinavyoweza kuwezesha maendeleo yenye sifa bora ya tasnia ya utalii wa kitamaduni ya maeneo na wilaya husika.

Alisema, kwa kujikita katika chapa ya utalii wa kitamaduni ya “Hao Zai Honghe, Honghe Hao Zai” na IP kuu “Makazi kwenye Honghe: Mwaliko kutoka Mkuu wa Kijiji”, pande hizo mbili zitaeleza kwa bidii simulizi za utalii wa kitamaduni wa Honghe kwa hadhira ya kimataifa, zikilenga kuifanya Honghe kuwa kivutio cha utalii na wa kukaa kwa muda mrefu kwa watumiaji wa mtandao wa ndani na nje ya China.

Siku hiyo pia shughuli ilizinduliwa ili kukusanya kaulimbiu ya kuitangaza Honghe kutoka duniani kote, ikiwa na kichwa cha “Kufikiria Honghe kwa Sentensi Moja”. Shughuli hiyo inawaalika watumiaji wa mtandao kutumia ubunifu na maneno yao kuandika maelezo yenye kuvutia zaidi kwa ajili ya eneo hilo la Honghe, hali ambayo itaendelea kuzidisha zaidi utambulisho wa chapa yake “Hao Zai Honghe, Honghe Hao Zai.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha