Lugha Nyingine
Fundi wa kike ahakikisha usalama wa treni katika Mji wa Tianjin kaskazini mwa China (3)
![]() |
| Li Weijia akiwa amepumzika kwenye sehemu ya matengenezo ya karakana ya treni za mwendo kasi (EMU) mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Julai 31, 2026. (Xinhua/Li Ran) |
TIANJIN - Wakati wa pilika nyingi za usafiri wa majira ya joto, mafundi zaidi ya mia moja wa treni za mwenda kasi (EMU) wanafanya kazi kwa zamu kwenye karakana ya EMU muda wote huko Tianjin kaskazini mwa China ili kuhakikisha kila treni imekaguliwa kwa kina na iko tayari kwa kutoa huduma.
Miongoni mwao ni Li Weijia, fundi wa kike aliyezaliwa mwaka 1998. Li anakagua kwa umakini saketi na vipuri, pasipo kuacha hatari yoyote ya usalama inayoweza kutotea bila kubainika. Tangu ajiunge na kazi za reli, Li siku zote anajikita katika kuongeza ujuzi wa kiufundi. Mwaka 2023, alishinda nafasi ya tano kwenye mashindano ya ujuzi wa kiufundi yaliyoandaliwa na kundi la Beijing la Shirika la Reli la China.
Mwaka huu, Li anajitahidi kuwakilisha kundi la Beijing la Shirika la Reli la China kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa ya ujuzi wa kiufundi ya Kundi la Reli la China. Kadri uteuzi wa washiriki wa mwisho unavyokaribia, anafanya kila kazi ya matengenezo kwa makini zaidi, akijitahidi kukamilisha vizuri kazi zote hata kazi ndogondogo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




