Waigizaji waonesha hali ya wakazi kuwaaga askari wa Jeshi Jekundu kushiriki kwenye Safari Ndefu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 04, 2026
Waigizaji waonesha hali ya wakazi kuwaaga askari wa Jeshi Jekundu kushiriki kwenye Safari Ndefu
Waigizaji wakifanya igizo fupi lenye kichwa cha "Kwaheri," katika Wilaya ya Yudu ya Mji wa Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China, Julai 28, 2026. (Picha na Xiao Liang/Xinhua)

Kwenye kivuko katika Wilaya ya Yudu ya Mji wa Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi, China, maonesho ya igizo fupi yanafanywa kila baada ya siku chache. Igizo hilo, lenye kichwa cha "Kwaheri," linaonesha hali ambayo katika majira ya mpukutiko ya mwaka 1934, wakazi wa wilaya hiyo ya Yudu waliaga kikosi cha jeshi kilichoongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kufunga Safari Ndefu.

Watu karibu 300 wa kujitolea kutoka sekta mbalimbali wanashirikiana na wasanii zaidi ya 20 ili kuwaletea watu igizo hilo. Tangu lilipoanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza hadharani mwaka 2021, igizo hilo la "Kwaheri" limeonyeshwa zaidi ya mara 800.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha