Lugha Nyingine
ChinaVumbuzi | Lifti ya kwenye ukingo wa mwamba yaanza kufanya kazi ili kurahisisha safari za wanafunzi kwenda shule mkoani Yunnan, China

Picha iliyopigwa Julai 31, 2026 ikionyesha lifti mbili za kwenye ukingo wa mwamba kwenye Genge Kubwa la Mto Nizhu katika Kijiji cha Nizhuhe cha Tarafa ya Puli, Mji wa Xuanwei, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua)
Lifti ya kwenye ukingo wa mwamba yenye urefu wa mita 288 imeanza kufanya kazi hivi karibuni kwenye Genge Kubwa la Mto Nizhu katika Kijiji cha Nizhuhe cha Tarafa ya Puli, Mji wa Xuanwei, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, sambamba na nyingine ya aina yake ambayo imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 2022. Hatua hiyo inatarajiwa kurahisisha zaidi safari za wanafunzi wenyeji kwenda shule zao.
Kijiji hicho cha Nizhuhe ni kijiji kidogo kilicho kwenye bonde refu lililochongwa na Mto Nizhu unaotiririka kutoka kusini hadi kaskazini. Hapo awali, njia fupi zaidi kutoka chini ya bonde hilo hadi juu ya mlima ilikuwa njia ya upande wa ukingo wa mwamba, na safari ya kwenda na kurudi ilichukua saa karibu sita. Watoto na wazazi wao walilazimika kufanya safari hiyo ngumu angalau mara moja kila baada ya siku 10.
Mwaka 2022, mabadiliko makubwa yalikuja katika safari hiyo yenye changamoto. Eneo la kivutio cha watalii la Genge Kubwa la Mto Nizhu lilikamilika na kufunguliwa, huku lifti ya kwenye ukingo wa mwamba yenye urefu wa mita 268 na mfumo wa gari la kebo vikianza kufanya kazi. Vifaa hivyo vimepatikana bila malipo kwa wanakijiji wenyeji.
Leo, mchanganyiko wa magari ya usafiri wa watalii, lifti na magari ya kebo umefupisha safari hiyo ya wanafunzi kwenda shuleni hadi dakika takriban 30. Njia mahsusi pia imewekwa kwa ajili ya wanafunzi, huku maafisa wa polisi na wafanyakazi mahsusi wakiwa walinzi wao kwenye safari hizo.

Picha iliyopigwa Julai 31, 2026 ikionyesha lifti mbili za kwenye ukingo wa mwamba kwenye Genge Kubwa la Mto Nizhu katika Kijiji cha Nizhuhe cha Tarafa ya Puli, Mji wa Xuanwei, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 31, 2026 ikionyesha lifti ya kwenye ukingo wa mwamba (kushoto) iliyoanza kufanya kazi hivi karibuni kwenye Genge Kubwa la Mto Nizhu katika Kijiji cha Nizhuhe cha Tarafa ya Puli, Mji wa Xuanwei, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 31, 2026 ikionyesha lifti mbili za kwenye ukingo wa mwamba kwenye Genge Kubwa la Mto Nizhu katika Kijiji cha Nizhuhe cha Tarafa ya Puli, Mji wa Xuanwei, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma