Lugha Nyingine
Beijing yateuliwa kuwa Mji Mkuu wa Ujenzi wa Majengo Duniani wa UNESCO-UIA 2029

Khaled Ahmed El-Enany Ali Ezz akizungumza baada ya kushinda uchaguzi wa mgombea wa nafasi ya mkurugenzi mkuu wa UNESCO jijini Paris, Ufaransa, Oktoba 6, 2025. (Xinhua/Zhang Baihui)
PARIS – Mji wa Beijing wa China umeteuliwa kuwa Mji Mkuu wa Ujenzi wa Majengo Duniani wa UNESCO-UIA (Umoja wa Kimataifa wa Wasanifu Majengo) 2029, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetangaza jana Jumatano.
Uteuzi huo umefuata pendekezo la Kamati ya Pamoja ya Mji Mkuu wa Ujenzi wa Majengo Duniani.
Mradi wa Mji Mkuu wa Ujenzi wa Majengo Duniani ulioanzishwa kwa pamoja na UNESCO na UIA, unasisitiza kazi kubwa muhimu ya ujenzi wa majengo, mipangilio ya miji, utamaduni na mali za urithi katika kusukuma mbele maendeleo endelevu ya miji. Kila baada ya miaka mitatu, UNESCO linateua mji mwenyeji wa Mkutano wa Dunia wa UIA kuwa Mji Mkuu wa Ujenzi wa Majengo Duniani wa UNESCO-UIA.
Kwa mujibu wa UNESCO, Beijing imechaguliwa kwa "uwezo wake wa kipekee wa kuunganisha mali yake ya urithi ambayo ni moja ya mali za urithi za majengo mengi zaidi duniani, na matarajio yake ya kuelekea siku za baadaye juu ya maendeleo endelevu ya miji.
UNESCO imetoa habari ikisema kuwa, "Mpangilio wa kihistoria wa mjini, miradi yenye mafanikio ya ujengaji upya na utamaduni wenye nguvu hai wa ujenzi wa majengo vinaonyesha namna mali ya urithi, uvumbuzi na maisha ya maeneo ya wakazi kuhimizana na kufanya juhudi za pamoja za kujenga mji kuwa wenye nguvu ya uhimilivu na unaofaa kuishi kwa watu."

Upinde wa mvua ukionekana angani baada ya mvua kunyesha mjini Beijing, Agosti 3, 2026. (Xinhua/Du Juanjuan)
Kwa kutazama siku za baadaye kwa Beijing 2029, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Khaled El-Enany akitoa habari moja ameeleza imani yake kwamba mali ya urithi wa majengo pekee yake ya ajabu ya mji huo, mabadiliko ya mji yanayojaa nguvu hai pamoja na matarajio yake ya kutupia macho siku za baadaye yatahamasisha mazungumzo mapya ya kimataifa juu ya nguvu ya ujenzi wa majengo.
Rio de Janeiro, Brazili, ilikuwa mji wa kwanza kuteuliwa kuwa Mji Mkuu wa Ujenzi wa Majengo Duniani wa UNESCO-UIA mwaka 2020, ikifuatiwa na Copenhagen na Barcelona.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



