Siku 100 kuelekea APEC: Machaguo ya kijani ya Mji wa Shenzhen, China yapongezwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 11, 2026
Siku 100 kuelekea APEC: Machaguo ya kijani ya Mji wa Shenzhen, China yapongezwa
Picha hii iliyopigwa Agosti 10, 2026 ikionyesha muonekano wa Kituo cha Michezo cha Shenzhen Bay, kikiwa na bango la matangazo linaloonyesha kuhesabiwa kwa siku 100 kuelekea Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC), Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Liang Xu)

SHENZHEN - Miongo kadhaa iliyopita, Mji wa Shenzhen wa China ambao mwaka huu utakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) ulifanya chaguo lisilo la kawaida la kupanga kulinda mikoko katika Eneo la Futian la mji huo, ukihamisha barabara ya pwani iliyokuwa imepangwa kujengwa umbali wa mita 260 kaskazini.

Hatua hiyo inakusudia kulinda msitu wa asili wa mikoko, kwa mujibu wa Bao Daming, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Kituo cha Kimataifa cha Mikoko (IMC) chenye makao makuu mjini Shenzhen. Kwa Bao, uamuzi huo unaakisi mbinu ya mji huo wa kisasa wa kusini mwa China katika kuwianisha maendeleo ya mjini na uhifadhi wa ikolojia.

Mbinu hiyo ilionyeshwa kwenye Mkutano wa Mawaziri wa APEC wa 2026 juu ya Misitu uliofanyika Shenzhen hivi karibuni. Wawakilishi kutoka nchi 21 walijadili usimamizi endelevu wa misitu, uhifadhi wa mikoko na kaboni ya bluu, bioanuwai za mjini, usimamizi bora wa kisasa wa ikolojia na biashara halali ya mazao ya misitu. Walisaini taarifa ya pamoja inayoweka mielekeo kwa ajilli ya ushirikiano wa kina zaidi wa kikanda.

Jana Jumatatu, Shenzhen iliadhimisha siku 100 kuelekea Mkutano wa Viongozi wa Kiuchumi wa APEC 2026, na kuleta ufuatiliaji kwa mara nyingine tena kwa vitendo vya kiikolojia vya mji huo mwenyeji. Shenzhen inapoelekea kwenye mkutano huo, vitendo vyake vya kiikolojia pia vinachangiwa na kujadiliwa miongoni mwa nchi za Asia-Pasifiki.

Mji huo unafungua maeneo yanayojihusisha na ulinzi wa mikoko, urejeshaji wa mito na shoroba za ikolojia kwa maafisa wa misitu na timu za kiufundi zilizoko ziarani mjini humo kutoka nchi za APEC. Pia inafanya kazi kupitia IMC katika utafiti wa pamoja kuhusu urejeshaji wa mikoko wa kuvuka-mipaka na uanzishaji wa vigezo vya kaboni ya bluu.

Eduardo Pedrosa, mkurugenzi mtendaji wa Sekretarieti ya APEC, amesema mbinu hiyo ya Shenzhen ya kuchanganya maendeleo ya mjini na uhifadhi wa mikoko inaweza kutumika kama marejeleo kwa miji kote Asia-Pasifiki.

"Inavutia kuona namna Shenzhen imeendelea katika kipindi cha miaka 20 iliyopita," amesema. "Kile ambacho tumeona ni minara mingi, majengo marefu, maendeleo ya mjini, lakini pia ni maeneo makubwa ya kijani ... bila shaka lipo eneo la mikoko lililolindwa vilevile."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha