Mkoa wa Hainan, China waongeza juhudi za kujenga mahali pa utalii na manunuzi pa kiwango cha juu cha maendeleo duniani (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 14, 2026
Mkoa wa Hainan, China waongeza juhudi za kujenga mahali pa utalii na manunuzi pa kiwango cha juu cha maendeleo duniani
Watalii wakitembelea eneo la mambo ya baharini la Atlantis Sanya, mkoani Hainan, kusini mwa China, Januari 15, 2026. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

Mkoa wa Hainan, kusini mwa China unaongeza juhudi za kujenga mahali pa utalii na manunuzi pa kiwango cha juu duniani kama sehemu muhimu ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan. Na pia unatafuta njia mpya ya kuelekea maendeleo yenye sifa bora ya uchumi wake wa walaji unaoongozwa na sekta ya utalii, ambao una sifa za kipekee za kisiwa hicho.

Hainan unakadiriwa kupokea watalii wa ndani na wa kimataifa wapatao milioni 154 kila mwaka ifikapo mwaka 2030, ambapo mapato yanayotokana na utalii yatafikia yuan bilioni 363 (dola karibu bilioni 53.83 za Marekani).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha