Lugha Nyingine
Jumba la makumbusho ya sayansi na teknolojia la Shanghai, China lakaribisha mtembeleaji wa milioni 100 (6)
SHANGHAI - Jumba la Makumbusho ya Sayansi na Teknolojia la Shanghai mashariki mwa China limekaribisha mtembeleaji wake wa milioni 100 jana Jumanne, wakati ambapo wasafiri wanaozidi kuwa wengi wanaifanya sayansi na teknolojia kuwa sehemu ya likizo zao.
Zhang Zhiheng, mvulana kutoka Mkoa wa Shandong mashariki mwa China, ndiye mtembeleaji huyo muhimu. Ametembelea jumba hilo la makumbusho pamoja na wazazi wake katika siku ya pili ya safari yake ya kwanza kwenda Shanghai.
Tangu lilipofungua milango yake kwa umma mwishoni mwa 2001, jumba hilo la makumbusho limekua na kuwa moja ya maeneo maarufu zaidi ya kutembelewa ya kisayansi na kielimu ya China. Kupitia shughuli na programu mbalimbali za sayansi na teknolojia, bado linaendelea kuwa na azma katika kuhimiza uelewa wa kisayansi wa umma na kuchochea udadisi kwa watembeleaji wa rika zote.
Baada ya kufungwa kwa miaka zaidi ya miwili kwa ajili ya maboresho, jumba hilo la makumbusho lilifunguliwa tena mapema mwaka huu. Sasa linajumuisha matawi mawili: Jumba la Makumbusho ya Elimu Viumbe la Shanghai na Jumba la Makumbusho ya Astronomia la Shanghai.
Kipindi cha nyuma mwaka 2001, idadi ya raia wa China wenye uelewa wa kisayansi ilikuwa asilimia 1.4 pekee, na takwimu hiyo iliongezeka hadi asilimia 16.74 ilipofika mwaka 2025, kwa mujibu wa takwimu rasmi.
Kadri shauku ya umma katika sayansi inavyozidi kuongezeka, utembeleaji kwenye majumba ya makumbusho ya sayansi na teknolojia umekuwa sehemu ya maisha ya kila siku.
Kwa familia nyingi, majumba ya makumbusho yamekuwa mahali maarufu pa kutembelea wakati wa likizo na wikendi, hali ambayo inawapa watoto fursa za kupanua maarifa yao na kupanua upeo wao.
"Mabadiliko makubwa ninayohisi wakati wa kutembelea kwangu jumba la makumbusho ni kwamba sayansi na teknolojia vinaendelea kupiga hatua," amesema Zheng Qina, mtembeleaji aliyezaliwa baada ya miaka ya 90 kutoka Shanghai. Alikuwa na umri wa miaka tisa alipotembelea jumba hilo la makumbusho mwaka 2001. Leo, mtoto wake wa miaka mitano pia ni mtembeleaji wa mara kwa mara.
Mwenendo huo pia unaenea kwa wasafiri wa kimataifa. Huku utalii wa raia wa kigeni wanaoingia China ukipata kasi kufuatia sera za viza zilizorahisishwa, majumba ya makumbusho ya sayansi yameibuka kuwa kivutio kinachozidi kuwa maarufu kwa watembeleaji wa ng'ambo wanaotafuta kutazama kwa karibu zaidi maendeleo ya kiteknolojia ya nchi hiyo.
Kutoka Januari hadi Julai mwaka huu, Jumba la Makumbusho ya Sayansi na Teknolojia la Shanghai na matawi yake hayo mawili yalipokea watembeleaji wa kigeni karibu 200,000, wakichukua asilimia karibu 5 ya idadi ya jumla ya watembeleaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




