Lugha Nyingine
Picha za zamani zabeba ushuhuda kwenye Muujiza wa Chuma wa Reli ya Qinghai-Xizang (6)
![]() |
| Kundi la punda pori wa kitibeti wakirandaranda karibu na Reli ya Qinghai-Xizang, tarehe 24, Oktoba, 2009. (Picha na Hou Deqiang/Xinhua) |
Tarehe 1, Julai, mwaka 2026 ilikuwa maadhimisho ya miaka 20 tangu Reli nzima ya Qinghai-Xizang nchini China ilipoanza kufanya kazi.
Ujenzi wa sehemu ya Xining-Geermu ya reli hiyo ulianza Septemba, 1958. Baada ya kupitia vipindi vya upigaji hatua kwa polepole, kusimamishwa kwa kazi ya ujenzi na kuanzishwa tena, sehemu hiyo hatimaye Mei 1, 1984 ilianza kutumika. Mnamo tarehe 29, Juni, 2001, baada ya raundi kadhaa za kuthibitisha uwezekano, ujenzi wa sehemu ya Geermu-Lhasa hatimaye ulianza rasmi.
Tarehe 1 Julai, 2006 sehemu ya Geermu-Lhasa ya Reli hiyo ya Qinghai-Xizang ilianza kufanya kazi, ikimaanisha kukamilika na kufunguliwa kwa njia nzima ya reli hiyo yenye urefu wa jumla wa kilomita 1956, kutoka Mji wa Xining hadi Mji wa Lhasa nchini China.
Njia nzima ya Reli ya Qinghai-Xizang inapita kilomita 550 za maeneo ya ardhi iliyoganda kwa miaka mingi, na kilomita 960 za ardhi ya miinuko ya juu – maeneo yanayozidi mita 4,000 kutoka usawa wa bahari ambayo mara nyingi ni yasiyofaa kwa maisha. Ujenzi wa reli hiyo ulizishinda changamoto tatu zinazotambuliwa kwa ugumu duniani, ambazo ni: ardhi iliyoganda kwa miaka mingi, baridi kali kupitiliza na oksijeni chache, na udhaifu wa kiikolojia.
Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, reli hiyo ambayo pia hutajwa kwa jina la “Njia ya Kuelekea Anga Inayoleta Furaha” imehuisha uwanda huo wa juu wa ardhi iliyoganda, kushuhudia mabadiliko yake makubwa, na kubeba ndoto za vizazi kuelekea mustakabali mzuri zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




