Daktari kijijini ajitolea kulinda afya ya watu wote kijijini katika siku zote za miongo kadhaa iliyopita (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 19, 2026
Daktari kijijini ajitolea kulinda afya ya watu wote kijijini katika siku zote za miongo kadhaa iliyopita
Wang Ju (kushoto) akizungumza na mwanakijiji wakati akiwa njiani kwenda nyumbani kwa watu kupeleka dawa katika Kijiji cha Lianghe cha Mji Lianghekou wa Wilaya ya Zigui ya Yichang, Agosti 16, 2026. (Xinhua/Du Zixuan)

Wang Ju, daktari mwenye umri wa miaka 59 wa Kijiji cha Lianghe cha Mji Lianghekou wa Wilaya ya Zigui mkoani Hubei, katikati mwa China, ingawa yeye ni mtu mwenye urefu wa mita 1.28 tu na uzito wa kilo 32 kutokana na tatizo la kudumaa, lakini ametoa matibabu na huduma ya afya kwa watu wote wa kijiji chake katika siku zote za miongo minne iliyopita.

Alipokuwa kijana, wanakijiji wenzake walimpa uangalizi mwingi, jambo ambalo lilimtia moto kusoma udaktari na kulipa wema kwa jamii yake. Baada ya kuhitimu kutoka shule ya afya, alirudi kijijini humo kutekeleza jukumu la kutoa matibabu ya kimsingi na huduma za afya.

Nyumba katika Kijiji cha Lianghe zimetawanyika katika sehemu mbalimbali za milimani na barabara ni ngumu kupitika. Awali, Wang aliwatembelea watu majumbani kwao kwa miguu tu. Baadaye aliagiza pikipiki maalumu iliyopunguzwa ukubwa yenye fremu ya urefu wa sentimita 50 pekee, iliyoundwa mahsusi kwa urefu wake.

Katika miaka 38 iliyopita, Wang amewatembelea wanakijiji nyumbani kwao kwa mara zaidi ya 6,000, ambapo hata pikipiki nne ziliharibika na jozi zaidi ya 100 za viatu kuchakaa kwa sababu ya matumizi yake ya mara kwa mara. Kwake yeye, kuwa daktari si kazi tu, bali ni ahadi yake ya kila siku ya kulinda afya ya watu ambao awali waliwahi kumpa uangalizi mwingi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha