ChinaVumbuzi | China yarusha Roketi ya Zhuque No. 3, ikifanikisha urejeshwaji wake wa kwanza wa roketi ardhini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 20, 2026
ChinaVumbuzi | China yarusha Roketi ya Zhuque No. 3, ikifanikisha urejeshwaji wake wa kwanza wa roketi ardhini
Roketi ya Zhuque No.3 Y2 ikirushwa kutoka kwenye eneo la majaribio ya uvumbuzi wa vyombo vya anga ya juu vya kibiashara la Dongfeng kaskazini magharibi mwa China, Agosti 19, 2026. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)

JIUQUAN - China imerusha Roketi ya Zhuque No.3 Y2, ambayo ni roketi inayoweza kutumika tena ya Zhuque No.3 jana Jumatano asubuhi, ikifanikisha urejeshwaji wa mara ya kwanza kwa ngazi ya kwanza ya roketi kwenye ardhi, ambapo roketi hiyo ilirushwa majira ya saa 1:35 asubuhi (Saa za Beijing) kutoka kwenye eneo la majaribio ya uvumbuzi wa vyombo vya anga ya juu vya kibiashara la Dongfeng kaskazini magharibi mwa China.

Sekunde takriban 137 baada ya kurushwa kwa roketi hiyo, ngazi ya kwanza na ya pili ya roketi vilitengana. Ngazi ya kwanza kisha iliingia katika kipindi chake cha kurudishwa kwa mpango uliowekwa, na kukamilisha mfululizo wa matendo muhimu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha hali ya kuruka kwenye anga ya juu, kupunguza msukumo wa kasi ya kuingia tena kwa ajili ya kurudishwa kwenye ardhi, kudhibiti uwiano wa hali ya kuruka angani, kupunguza mwendo kasi ya kurudishwa na kunyoosha miguu kwa ajili ya kutua kwenye ardhi.

"Kadri roketi ilivyokuwa ikipita kwenye anga ya chini, bado ilikuwa ikiruka kwa mwendo kasi. Kulikuwa na fursa moja tu katika mchakato kama huo, kama vile tu kufanikisha hali ya kuegesha kwa kasi ya juu kwa jaribio la mara moja," amesema Dai Zheng, kiongozi mkuu wa mradi wa Roketi ya Zhuque No.3.Urejeshwaji huo wa roketi kwenye ardhi umekamilishwa kwa mpango uliowekwa, ambapo ngazi ya kwanza ya roketi ikitua vizuri katika sehemu iliyopangwa kwa ajili ya urejeshwaji wa roketi katika Wilaya ya Minqin, mkoani Gansu, kaskazini magharibi mwa China. Ngazi ya pili iliendelea kuruka na kupeleka satalaiti ya Honghu No. 03 kwenye obiti iliyopangwa. Jukumu hilo la kuruka limetekelezwa kwa mafanikio makubwa.

Jukumu hilo linafuatia urejeshwaji kwa mafanikio wa kutumia wavu baharini wa ngazi ya kwanza ya Roketi ya Changzhen No.10B Tarehe 10, Julai.

Hii ni mara ya kwanza kwa China kurejesha ngazi ya kwanza ya roketi kwenye ardhi kwa kutumia miguu ya kutua inayoweza kunyoosha, hii ikionesha wazi mafanikio makubwa ya China katika teknolojia ya roketi inayoweza kutumika tena.

Roketi ya Zhuque No.3, iliyoundwa na kampuni ya vyombo vya anga ya juu vya kibiashara ya LandSpace ya China, imeidhinishwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Anga ya Juu ya China (CNSA), roketi hiyo ni ya kizazi kipya inayoendeshwa kwa nguvu ya kimiminika cha oksijeni-methani kwa ajili ya urushwaji wa gharama nafuu, wenye uwezo mkubwa wa uchukuzi na wa masafa ya juu.

Wataalamu wa mambo ya anga ya juu wanaona kuwa, uthibitishaji huo wenye mafanikio wa mpango wa teknolojia ya Roketi ya Zhuque No.3 inayounganisha kazi za msukumo wa kimimika cha oksijeni-methane, bodi la chuma cha pua kisichoweza kupata kutu pamoja na kutua na kurejeshwa kwa wima, kutasaidia kuharakisha mpangilio wa kundi la satalaiti za China kwenye obiti ya chini.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha